Na Lucy Ngowi
DODOMA: KATIBU Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara, leo Juni 22, 2026 ametembelea banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika Maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Akiwa katika banda hilo, Profesa Kahyarara alipatiwa maelezo kuhusu juhudi za TASAC katika kuhakikisha usalama, ulinzi na ubora wa huduma za usafiri wa majini kwa wananchi.

Baada ya kupata maelezo hayo, Profesa Kahyarara aliipongeza TASAC kwa kushiriki maonesho hayo na kutumia jukwaa hilo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu na huduma zake.
Amesema elimu hiyo inasaidia kuongeza uelewa wa umma na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi na wananchi.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu” yalianza rasmi Juni 16, 2026 na yanatarajiwa kufikia tamati kesho Juni 23, 2026.

