MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TPHPA Yasisitiza Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wakulima
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TPHPA Yasisitiza Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wakulima
Habari

TPHPA Yasisitiza Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wakulima

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imeendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wakulima na wafanyabiashara, ikieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuongeza uzalishaji wa mazao na kulinda afya ya binadamu pamoja na mazingira.
Akizungumza katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, Mkaguzi wa Biashara ya Viuatilifu wa TPHPA, Ereneus Mwinuka, amesema wakulima wengi bado wanakabiliwa na changamoto ya kutotambua viuatilifu vinavyofaa kwa ajili ya kudhibiti wadudu na magonjwa yanayoshambulia mazao yao.
Amesema mamlaka hiyo inatumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kusoma taarifa zilizopo kwenye lebo za viuatilifu kabla ya matumizi, ili kuhakikisha wanachagua bidhaa sahihi kulingana na aina ya kisumbufu wanachotaka kudhibiti.
Kwa mujibu wa Mwinuka, matumizi ya viuatilifu visivyofaa yanaweza kusababisha hasara kwa mkulima kutokana na kushindwa kudhibiti tatizo husika, hivyo ni muhimu kutambua kwanza kisumbufu kabla ya kufanya ununuzi wa bidhaa.
Aidha, amewataka wakulima kuhakikisha wanatumia viuatilifu vilivyosajiliwa na kuthibitishwa na TPHPA kwa kuangalia namba za usajili pamoja na tarehe ya mwisho wa matumizi ili kuepuka matumizi ya bidhaa zisizo salama au zisizo na ufanisi.
Mbali na wakulima, TPHPA pia imekuwa ikitoa elimu kwa wafanyabiashara wa viuatilifu kuhusu taratibu za biashara hiyo, ikiwemo masharti ya kupata leseni na wajibu wao wa kuwapa wakulima ushauri sahihi kuhusu matumizi ya bidhaa wanazouza.
Mwinuka amesema mwitikio wa wananchi kutembelea banda la mamlaka hiyo umekuwa mkubwa, jambo linaloonyesha kuongezeka kwa uelewa na hamasa ya kutafuta taarifa sahihi kuhusu matumizi ya viuatilifu.
Ameeleza kuwa wageni wengi waliotembelea banda hilo wamepata maarifa mapya yatakayowasaidia kufanya maamuzi bora wakati wa kununua na kutumia viuatilifu katika shughuli za kilimo.

You Might Also Like

TEA Yawaalika Wananchi Kujifunza SDF Unavyofanya Kazi

BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha

TASAC Yapiga Marufuku Kampuni Binafsi Kusafirisha Shehena Hatarishi Za Migodini

OCPD Nguzo Kuu ya Utungaji Sheria – Dkt. Ndumbaro

Mwongozo wa Mafunzo Elekezi Kwa Walimu Wapya Kazini Mbioni Kukamilika

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article BRELA Yahamasisha Urasimishaji wa Biashara kwa Ukuaji wa Uchumi
Next Article Magereza Yaomba Jamii Kuwapokea Wafungwa Wanaorejea Kutumikia Taifa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Hananja Awataka Vijana Kufikiri Mara Mbili Kabla ya Kufuata Wito wa Maandamano
Habari June 18, 2026
June 18, 2026
Habari June 18, 2026
Magereza Yaomba Jamii Kuwapokea Wafungwa Wanaorejea Kutumikia Taifa
Habari June 18, 2026
BRELA Yahamasisha Urasimishaji wa Biashara kwa Ukuaji wa Uchumi
Habari June 18, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?