MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: BRELA Yahamasisha Urasimishaji wa Biashara kwa Ukuaji wa Uchumi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > BRELA Yahamasisha Urasimishaji wa Biashara kwa Ukuaji wa Uchumi
Habari

BRELA Yahamasisha Urasimishaji wa Biashara kwa Ukuaji wa Uchumi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
Dodoma:WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewataka wafanyabiashara nchini kuhakikisha wanarasimisha biashara zao kwa kuzisajili rasmi ili kuongeza fursa za ukuaji, kupata masoko mapya na kuimarisha ushindani wa biashara zao.
Wito huo umetolewa na Ofisa Usajili wa BRELA, Yusuph Mwasakafyuka, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Amesema usajili wa biashara una manufaa makubwa kwa wafanyabiashara kwani huwapa utambulisho rasmi, hulinda chapa zao za biashara na kuwajengea uaminifu kwa wateja pamoja na wadau wengine wa maendeleo.
Mwasakafyuka amesema BRELA inatumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo, sambamba na kusajili biashara na kutoa vyeti papo kwa papo kwa waombaji wanaokidhi vigezo.
Ameeleza kuwa taasisi hiyo inasimamia sheria zinazohusu usajili wa makampuni, majina ya biashara, alama za biashara, leseni za viwanda, leseni za biashara za Kundi A na usajili wa hataza.
Kwa mujibu wake, mwitikio wa wananchi umeendelea kuongezeka tangu kuanza kwa maonesho hayo, ambapo mamia ya watu wamejitokeza kupata huduma na ushauri kuhusu usajili wa biashara na masuala mengine yanayohusiana na urasimishaji wa shughuli za kiuchumi.
Aidha, amesema wataalamu wa BRELA wamekuwa wakitoa msaada kwa wateja wanaokabiliwa na changamoto katika matumizi ya mfumo mpya wa usajili, hususan wale waliowasilisha taarifa zisizo sahihi wakati wa kujisajili.
Amesisitiza kuwa biashara zilizosajiliwa huwa na nafasi kubwa ya kupata huduma za kifedha kutoka benki na taasisi nyingine za mikopo, jambo linalosaidia kuongeza mtaji na kupanua shughuli za uzalishaji.
“Urasimishaji wa biashara ni hatua muhimu katika kujenga biashara imara na yenye uwezo wa kushindana katika soko la ndani na nje ya nchi,” amesema.

You Might Also Like

Profesa Anangisye Atoa Neno Kwa Wahitimu

Hali Ya Ulinzi Na Usalama Wa Mipaka Ni Salama

Majukwaa YA Dini Yaimarishe Mapambano Dhidi ya Magonjwa Ya Mlipuko

TFRA yazindua Chama cha wafanyabiashara wa Mbolea

Wizara ya Maji: Uhifadhi Ziwa Victoria Unahitaji Ushirikiano, Uwekezaji Endelevu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article SELF Yahamasisha Wananchi Kunufaika na Mikopo Nafuu ya Maendeleo
Next Article TPHPA Yasisitiza Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wakulima
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Hananja Awataka Vijana Kufikiri Mara Mbili Kabla ya Kufuata Wito wa Maandamano
Habari June 18, 2026
June 18, 2026
Habari June 18, 2026
Magereza Yaomba Jamii Kuwapokea Wafungwa Wanaorejea Kutumikia Taifa
Habari June 18, 2026
TPHPA Yasisitiza Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wakulima
Habari June 18, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?