MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Teknolojia ya Kuvuna Sumu ya Nyuki Yafungua Fursa Mpya Tanzania
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Teknolojia ya Kuvuna Sumu ya Nyuki Yafungua Fursa Mpya Tanzania
Makala

Teknolojia ya Kuvuna Sumu ya Nyuki Yafungua Fursa Mpya Tanzania

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
4 Min Read

Na Lucy Ngowi

Sumu ya nyuki ni moja ya bidhaa adimu zenye thamani kubwa kiafya na kiuchumi duniani, lakini bado haijafahamika kwa kiwango kikubwa nchini Tanzania.

Bidhaa hiyo huvunwa kwa kutumia teknolojia maalumu bila kumuua nyuki, na hutumika katika utengenezaji wa dawa, vipodozi pamoja na tafiti mbalimbali za tiba.

Kadri dunia inavyoelekea kwenye matumizi ya teknolojia na ubunifu katika kilimo na afya, vijana wa Kitanzania wameanza kuona fursa mpya ndani ya sekta ya ufugaji nyuki kupitia uvunaji wa sumu ya nyuki.

Habari Picha 12215

Mkurugenzi wa kampuni ya Sensor Tanzania Ltd, Patrick Kitosi, anasema kampuni hiyo imejikita katika ubunifu wa mashine mbalimbali, ikiwemo mashine za kuvuna sumu ya nyuki kwa kutumia teknolojia ya kielektroniki.

Anasema ili kuvuna sumu hiyo, nyuki huchochewa kwa mshtuko mdogo wa umeme unaowafanya wajihami kwa kutoa sumu kwenye kifaa maalumu kilichowekwa kwenye mzinga.

Anasema sumu hiyo hukusanywa katika mfumo wa unga na kupimwa kwa gramu kabla ya kuuzwa sokoni.

“Teknolojia hii tuliianza kuifanyia utafiti tangu mwaka 2021. Tulibuni mfumo unaotumia sauti kuvuta nyuki karibu na kifaa, kisha hupata mshtuko mdogo wa umeme na kutoa sumu bila kuathiri maisha yao,” anasema Kitosi.

 

Habari Picha 12216

Kwa mujibu wake, sumu ya nyuki ina matumizi makubwa katika sekta ya afya, ikiwemo kusaidia kutengeneza dawa za magonjwa yanayohusiana na mishipa ya fahamu, misuli na baadhi ya maambukizi ya bakteria.

Anasema, nchi kama Algeria, India na China tayari zimewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye matumizi ya bidhaa hiyo.

Kwa maelezo yake, Tanzania ina wafugaji wengi wa nyuki, lakini wengi wao wamejikita zaidi kwenye uzalishaji wa asali huku wakikosa elimu na teknolojia ya kuvuna bidhaa nyingine zenye thamani kubwa kama sumu ya nyuki, nta, gundi na chavua.

“Changamoto kubwa si ukosefu wa nyuki, bali ni ukosefu wa teknolojia na masoko. Ndiyo maana sisi tukaamua kuwekeza kwenye ubunifu wa mashine ili wafugaji waweze kunufaika zaidi,” anasema.

Habari Picha 12218

Mbali na kuongeza kipato, uvunaji wa sumu ya nyuki pia una mchango katika utunzaji wa mazingira.

Kitosi anaeleza kuwa baada ya nyuki kutoa sumu, hulazimika kutafuta virutubisho zaidi kutoka kwenye maua ili kurejesha nguvu zake, hali inayoongeza uchavushaji wa mimea na kusaidia uzalishaji wa mazao.

Ubunifu huo unaonekana kwenda sambamba na dira ya maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2050 inayolenga kujenga uchumi wa kisasa unaotegemea maarifa, teknolojia na ubunifu.

Kupitia teknolojia hiyo, vijana wanapata ajira katika utengenezaji wa vifaa, huku wafugaji wakiongeza thamani ya shughuli zao.

Mwaka 2022, wabunifu hao walipata *mwega* wa Sh. Milioni 28 kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa ajili ya kuendeleza utafiti na utengenezaji wa vifaa hivyo.

Kitosi anasema soko la sumu ya nyuki lipo zaidi nje ya nchi kutokana na matumizi makubwa ya bidhaa hiyo katika viwanda vya dawa.

Habari Picha 12219

Hata hivyo, anabainisha kuwa wafugaji wengi bado wanahitaji kusaidiwa kupata masoko na elimu ya namna ya kuhifadhi bidhaa hiyo, kwani huhitaji mazingira yenye ubaridi ili isiharibike.

Anasema mzinga mmoja unaweza kutoa hadi gramu 1.5 za sumu kwa uvunaji mmoja, na mfugaji anaweza kuvuna mara kadhaa kwa mwezi endapo atatumia teknolojia sahihi.

Kwa sasa, kampuni hiyo inaendelea kuunganisha wafugaji na masoko huku ikihamasisha Watanzania kuona ufugaji nyuki kama biashara ya kisasa yenye bidhaa nyingi zaidi ya asali pekee.

Kadri dunia inavyohitaji bidhaa za asili kwa matumizi ya afya na tiba, ubunifu wa kuvuna sumu ya nyuki unaweza kuwa moja ya fursa mpya zitakazoibadilisha sekta ya ufugaji nyuki nchini na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa.

You Might Also Like

Mazao Bora Ya Kilimo Kutoka Tanzania Yavutia China

Profesa Ndunguru: Mtafiti Aliyejitoa Kusaidia Dunia Kupata Chakula Cha Baadae

Polisi Dar yashikilia watatu kwa mauaji ya mfanyakazi wa Kampuni ya Hope Recycling

Abubakar Assenga Aomba Ridhaa Ya Wananchi Wa Kilombero Wamchague Tena

Tujenge Jumuiya Yenye Mustakabali wa Pamoja kati ya China na Afrika – Wang Yi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article NIDA Kufanya Usajili Wa Watoto  Kuanzia Umri Wa Kuzaliwa,Kutoa Namba Maalum
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NIDA Kufanya Usajili Wa Watoto  Kuanzia Umri Wa Kuzaliwa,Kutoa Namba Maalum
Habari May 25, 2026
TPHPA Yatumia Mbinu za Kibaiolojia Kudhibiti Gugu Ziwa Victoria
Habari May 24, 2026
Wizara Ya Viwanda Kutekeleza Vipaumbele Saba, Ipo  Miradi Ya Viwanda Ya  Kimkakati
Habari May 22, 2026
Biashara 15 Hazitakiwi Kufanywa Na Wageni Ndani Ya Nchi
Habari May 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?