MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: JWTZ Kulipa Fidia Wananchi Waliochukuliwa Maeneo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > JWTZ Kulipa Fidia Wananchi Waliochukuliwa Maeneo
Habari

JWTZ Kulipa Fidia Wananchi Waliochukuliwa Maeneo

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Lyatuu, Dodoma
WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imesema imetenga sh bilioni 30 Kwa ajili ya kulipa fidia Kwa maeneo yote ya wananchi,fedha ambayo italipwa ndani ya bajeti ya Wizara hiyo 2026/2027.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Rhimo Nyansaho amesema hayo bungeni wakati akihitimisha hotuba ya bajeti yake.

Katika bajeti hiyo,Wizara inaomba kuidhinishiwa Sh trilioni 4.28 kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuimarisha ulinzi wa taifa, teknolojia za kijeshi na kuongeza uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Kuhusu fidia amesema fedha hizo zitalipwa na hazina katika kipindi hicho Cha bajeti na kwamba wananchi wamekuwa welewa wasio na vurugu hata pale maeneo yao yanachukuliwa na Jeshi.

Habari Picha 12123

Amewataka Wananchi kuwa sehemu ya kuzuia migogoro na zaidi kuwa na mapenzi na uzalendo na nchi yao.

Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo, amesema kati ya fedha hizo, Sh trilioni 3.85 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh bilioni 426.5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Dkt. Nyansaho alisema katika mwaka wa fedha 2026/27 wizara hiyo itatekeleza mpango na bajeti yake kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa 2026/27 hadi 2030/31, Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs), pamoja na mpango mkakati wa wizara na taasisi zake.

Amesema vipaumbele vya wizara hiyo vitajikita katika maeneo nane, yakiwemo kuimarisha jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa vya kijeshi, teknolojia ya mawasiliano pamoja na rasilimali watu.

Kuhusu mafunzo ya JKT amesema Katika kuhakikisha wahitimu wote wa Kidato cha Sita wanapata fursa ya kujiunga na mafunzo ya JKT, wizara imeendelea kuboresha miundombinu ya kambi ambapo kwa mwaka wa fedha 2025/26 vijana 60,000 walichukuliwa kw aajili ya kujiunga na JKT

Habari Picha 12124

Amesema Serikali inaendelea kufungua kambi mpya na kuboresha zilizopo ili kuwezesha JKT kuchukua vijana 140,000 ifikapo mwaka 2031, hatua itakayowezesha wahitimu wote wa Kidato cha Sita kupata nafasi ya mafunzo.

“Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea vijana uzalendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa na kuwapatia stadi za kazi na maisha ili waweze kujitegemea wanaporejea uraiani,” amesema.

Aidha, Serikali inapanga kuboresha mfumo wa mafunzo hayo kwa kuingiza zaidi elimu ya ufundi, kwakuwa sio kila kijana anayepitia JKT analenga kujiunga na vyombo vya ulinzi na usalama.

 

You Might Also Like

Serikali Kushughulikia Utitiri Wa Vyama Ndani Ya Sekta Binafsi

Hali Ya Ulinzi Na Usalama Wa Mipaka Ni Salama

Profesa Kabudi Atoa Maagizo Mazito Bodi Ya Ithibati Ya Waandishi Wa Habari

December 5, 2024

Makumbuli: Tunapinga kilimo cha bangi na mirungi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Timu Ya Bunge Yakabidhiwa Vifaa Vya Michezo
Next Article Utafiti wa Chakula Bora cha Kuku wa Nyama Watoa Tumaini kwa Wafugaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Utafiti wa Chakula Bora cha Kuku wa Nyama Watoa Tumaini kwa Wafugaji
Makala May 19, 2026
Timu Ya Bunge Yakabidhiwa Vifaa Vya Michezo
Habari May 19, 2026
Ndoinyo Aishauri Serikali Kurejesha Utalii Vijijini
Habari May 19, 2026
Nyavu za Plastiki Zatishia Afya za Watumiaji wa Samaki Ziwa Victoria
Habari May 19, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?