MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Utunzaji Ziwa Victoria Wasisitizwa kwa Mustakabali wa Uchumi, Mazingira
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Utunzaji Ziwa Victoria Wasisitizwa kwa Mustakabali wa Uchumi, Mazingira
Habari

Utunzaji Ziwa Victoria Wasisitizwa kwa Mustakabali wa Uchumi, Mazingira

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi, Mwanza
KATIBU Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria yenye makao yake Kisumu, Kenya, Dkt. Masinde Bwire, amesema bila kuchukua hatua muhimu za kisera, kisayansi na kiutendaji, Ziwa Victoria litaendelea kuharibika na kushindwa kuchangia ukuaji wa uchumi, maendeleo ya jamii pamoja na uhifadhi wa ikolojia.
Dkt. Bwire amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianzisha maadhimisho ya Siku ya Ziwa Victoria kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kulienzi, kulitunza na kulihifadhi ziwa hilo ambalo ni muhimu kwa maisha na uchumi wa watu wa ukanda huo.
Amesema Ziwa Victoria linakabiliwa na shinikizo kubwa la uchafuzi wa mazingira pamoja na matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali zake.
Ameeleza kuwa ukanda wa ziwa umebarikiwa kuwa na madini ya dhahabu, ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo na mazao ya viwandani, pamoja na mbuga na hifadhi kubwa kama Serengeti na Maasai Mara ambazo ni muhimu kwa uchumi wa nchi za Afrika Mashariki.
Aidha, amesema ziwa hilo linaunganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, hivyo kuwa kiungo muhimu cha biashara, usafirishaji na shughuli nyingine za kiuchumi, jambo linalofanya uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali zake kuwa wa lazima.
Kwa mujibu wa Dkt. Bwire, tafiti zilizofanywa na Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria zimebaini kuwepo kwa kiwango kikubwa cha uchafuzi wa maji katika maeneo mengi ya ziwa na fukwe zake.
Tafiti hizo zimeonyesha uwepo wa kemikali hatarishi ikiwemo zebaki (mercury), taka ngumu, plastiki pamoja na maji taka yanayotiririka kutoka majumbani na viwandani.
Ametaja baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi kuwa ni Mwanza, Geita, Musoma, Entebbe, Jinja, Homa Bay na Kisumu, ambapo taka ngumu hazizolewi kwa wakati na mvua zinaponyesha husombwa kuingia ziwani.
Pia amesema ukataji wa miti katika vyanzo vya maji umechangia mmomonyoko wa udongo na mchanga ambao husombwa na maji kuingia ziwani, hali inayoongeza kina cha maji na kusababisha baadhi ya fukwe kumezwa na maji.
Dkt. Bwire ameonya kuwa endapo hatua madhubuti hazitachukuliwa sasa, hali ya uchafuzi itaendelea kuongezeka na kuhatarisha uwepo wa ziwa hilo katika miaka ijayo.
“Kwa tafiti tunazozifanya, hali ikiendelea hivi, ndani ya miaka 50 hadi 80 ijayo tunaweza kupoteza uwezo wa kulirejesha Ziwa Victoria katika hali yake ya kawaida,” amesema Dkt. Bwire.

You Might Also Like

Wanafunzi 431, Watumishi 52 Watembelea TARI kujifunza Kilimo

Wakazi Wa Ntyuka Wataka Kiongozi Mchapakazi

CAG Aipongeza TARURA Kwa Ujenzi Wa Miundombinu

Uwepo mwongozo kupima wagonjwa zaidi

China Yafundisha Wanafunzi DIT kuzifikia fursa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Inzi Chuma: Suluhisho la Chakula cha Mifugo, Uhifadhi wa Mazingira
Next Article Nyavu za Plastiki Zatishia Afya za Watumiaji wa Samaki Ziwa Victoria
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Nyavu za Plastiki Zatishia Afya za Watumiaji wa Samaki Ziwa Victoria
Habari May 19, 2026
Inzi Chuma: Suluhisho la Chakula cha Mifugo, Uhifadhi wa Mazingira
Makala May 18, 2026
Ziwa Victoria Lanufaisha Watu Milioni 45 Afrika Mashariki – Mtanda
Habari May 18, 2026
Mbunge Ataka Vijiji Vinavyozunguka Mlima Kilimanjaro Kulipwa Fedha Za Uwajibikaji
Habari May 18, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?