MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Rais Samia Amkabidhi Tuzo Profesa Ndunguru kwa Kuinua Mapato, Maboresho TPHPA
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Rais Samia Amkabidhi Tuzo Profesa Ndunguru kwa Kuinua Mapato, Maboresho TPHPA
Habari

Rais Samia Amkabidhi Tuzo Profesa Ndunguru kwa Kuinua Mapato, Maboresho TPHPA

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
NJOMBE: RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtunuku tuzo ya Mfanyakazi Hodari Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe.
Profesa Ndunguru, anayewakilisha Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia na Taasisi za Utafiti (RAAWU), alijiunga na TPHPA mwaka 2023 na kuongoza mageuzi makubwa yaliyoifanya taasisi hiyo kuwa mfano barani Afrika.
Mafanikio hayo ni pamoja na kuboresha maabara na kuongeza uwezo wa uchambuzi wa viuatilifu, pamoja na kuunganisha ofisi 47 za mipakani katika mfumo mmoja.
Habari Picha 11952
Hatua hiyo imeongeza ufanisi na mapato kutoka Sh. Bilioni 14 mwaka 2023 hadi bilioni 69 ndani ya miezi minane (Julai 2025–Februari 2026).
Akizungumza katika sherehe hizo, Rais Samia aliwapongeza wafanyakazi wote kwa mchango wao katika kukuza uchumi na kuahidi kuendelea kuboresha maslahi yao.
“Serikali inatambua mchango wenu na itaendelea kuboresha maslahi pamoja na kulipa madai na kutafuta ajira zenye staha,” amesema.
Habari Picha 11953
Kwa upande wake, Profesa Ndunguru amesema ushindi huo unatokana na ushirikiano wa wafanyakazi na uongozi wa Serikali.
Ameeleza kuwa TPHPA sasa inawezesha vipimo vya ubora wa mazao kufanyika ndani ya nchi, hivyo kupunguza gharama na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya kimataifa.
Ameongeza kuwa mamlaka hiyo imeanza kutafuta masoko ya kimataifa kwa mazao ya kimkakati, ikiwemo kuwasaidia wazalishaji wa parachichi na viazi kupata soko nchini China.
Pia, mipango inaendelea ya kujenga maabara mpya Arusha na Makambako pamoja na kituo cha kuhifadhi mbegu za asili 10,000.
Aidha, amesema TPHPA itaendelea kushirikiana na wanahabari kupitia JOWUTA kuelimisha umma na kudhibiti uingizaji wa viuatilifu visivyoidhinishwa.
Habari Picha 11954
Profesa Ndunguru akiwa na washindi wa tuzo  hodari kitaifa wa Chama cha Wafanyakazi Katika Vyombo vya Habari (JOWUTA), Idda Mushi na Lucy Ngowi
Profesa Ndunguru pia ameahidi kufanyakazi na chama cha wafanyakazi katika vyombo vya Habari nchini(JOWUTA) kwa kuwajengea uwezo wanahabari juu ya kazi za Mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa JOWUTA Taifa, Mussa Juma amempongeza Profesa Ndunguru na wafanyakazi wote wa TPHPA Kwa kazi nzuri wanayofanya na pia ameshukuru TPHPA kuwa mmoja wa wafadhili wa zawadi za waandishi hodari mwaka 2026.

You Might Also Like

MNH Kuvuna Mifupa Kutengeneza Taya

Asha Moto Aibuka Kidedea Ubunge wa Viti Maalum Mtwara Kupitia CCM

Vijana Ni Chachu Ya Maendeleo Endelevu Wakiwezeshwa-Kikwete

Polisi Kuimarisha Ulinzi Nyumba Za Ibada Krismasi, Mwaka Mpya

Muhogo, viazi kuongezewa tija kwenye uzalishaji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mwandishi Lucy Ngowi Miongoni mwa Waliong’ara Mei Mosi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mwandishi Lucy Ngowi Miongoni mwa Waliong’ara Mei Mosi
Habari May 2, 2026
Tanzania yaendelea kuwa Shule ya Utumishi Barani Afrika,
Habari April 29, 2026
Wizara Ya Kilimo Yaomba Bunge Kuidhinisha Trilioni 1.1,Yaweka Mikakati Kuimarisha Sekta Hiyo
Habari April 28, 2026
NSSF Yafikia Trilioni 11.2, Hifadhi Skimu Yatajwa Kubadili Maisha ya Watanzania
Habari April 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?