MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Makampuni 100 kushiriki maonesho ya OSHA Njombe
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Makampuni 100 kushiriki maonesho ya OSHA Njombe
Habari

Makampuni 100 kushiriki maonesho ya OSHA Njombe

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
NJOMBE: ZAIDI ya makampuni 100, yakiwemo ya uchimbaji wa madini, yanatarajiwa kushiriki maonesho ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) yatakayofanyika katika viwanja vya Sabasaba, mjini Njombe.
Maonesho hayo yatafunguliwa rasmi Aprili 24 na kufikia kilele chake Aprili 29, mwaka huu 2026 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani pamoja na shamrashamra za Mei Mosi.
Akizungumza na waandishi wa habari wa Chama cha Waandishi wa Habari na Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Meneja wa OSHA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Wilbert Ngowi, amesema maandalizi yote yamekamilika.
Amesema pamoja na maonesho hayo, kutakuwa na utoaji wa tuzo kwa makampuni na taasisi zitakazofanya vizuri katika kuzingatia masuala ya usalama na afya kazini.
“Tunatarajia tuzo hizi zitatolewa Aprili 29 katika ukumbi wa Agrimet mjini Njombe, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi, Deus Sangu,” amesema Ngowi.
Aidha, OSHA imeandaa semina kwa wafanyakazi Aprili 27 zitakazojikita katika masuala ya kazi, afya na saikolojia, sambamba na michezo mbalimbali itakayofanyika katika kipindi chote cha maadhimisho hayo.
Ngowi amesema wamejipanga kuhakikisha maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu yanafanikiwa, huku akitoa wito kwa makampuni ambayo bado hayajakamilisha usajili kujitokeza mapema kupitia mfumo wa OSHA.
Kwa upande wake, JOWUTA imethibitisha kushiriki kwa mara ya kwanza katika maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa mwaka huu 2026 mkoani Njombe pamoja na  baadhi ya mikoa mingine nchini.

You Might Also Like

DC Atoa Wito kwa Tume ya Kurekebisha Sheria Kuzingatia Sheria Ndogondogo za Halmashauri

UTT AMIS Yazindua kampeni ya ‘Kijiwe Mchongo

Mdemu Azindua Utafiti Uliofanywa na FES Kwa Kushirikiana Na COTWU – T

Katoro Yapata Gari Jipya la Zimamoto, Kuwasili Februari 9

Watafiti Mradi Wa  AGRISPAK kutoka SUA Waanza Uandaaji Wa Vitabu Vidogo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ufaulu  Wa   Somo La Hisabati  Shida Ya Taifa- Wanu
Next Article Serikali Yatoa Mwelekeo Maandalizi AFCON 2027, Yaimarisha Miundombinu Nchini
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Sheria Ya  Kuzuia Shisha Kutungwa, Yabainika Kuwekwa Dawa Za Kulevya
Habari May 29, 2026
Waraibu Wa Dawa Za Kulevya 85,425  Wapatiwa Huduma Ya Tiba Nchini Kwa Mwaka 2025
Habari May 29, 2026
NHC Kuendelea Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Kimkakati Ya Ujenzi Wa Nyumba
Habari May 28, 2026
Kutokulipa Kodi Ya Pango La Ardhi Unakosa Sifa Za Kugombea Nafasi Za Uongozi
Habari May 28, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?