MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Amani, Maendeleo Haviwezi Kutenganishwa — Dkt. Nchimbi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Amani, Maendeleo Haviwezi Kutenganishwa — Dkt. Nchimbi
Habari

Amani, Maendeleo Haviwezi Kutenganishwa — Dkt. Nchimbi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema maendeleo ya kudumu hayawezi kupatikana bila amani, na kwamba amani ya kudumu haiwezi kupatikana bila maendeleo jumuishi na endelevu.
Amesema hayo kutokana na kauli mbiu ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika jijini Kinshasa Novemba 15, 2025, isemayo: ‘Kuimarisha Amani na Usalama kwa ajili ya Maendeleo Endelevu kwenye Eneo la Maziwa Makuu.’.
Habari Picha 10341
Dkt. Nchimbi amesema eneo la Maziwa Makuu limebarikiwa na utajiri mkubwa wa maliasili, zikiwemo madini adimu na rasilimali watu, lakini bado linakabiliwa na migogoro ya kisiasa ya muda mrefu inayochochewa na masuala mbalimbali kama uvunaji haramu wa maliasili.
Amesema migogoro hiyo imesababisha majanga ya kibinadamu, ikiwemo watu kukimbia makazi yao na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaotokana kwa kiasi kikubwa na uhalifu wa kivita.
Ameeleza kuwa sambamba na jitihada za kikanda na kimataifa zinazoendelea kudhibiti migogoro hiyo, Tanzania kama nchi muasisi wa ICGLR imehusika katika jitihada mbalimbali za kukomesha migogoro ndani ya kanda, ikiwemo kuchangia vikosi vya kulinda amani nchini DRC na kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi za SADC na EAC uliolenga kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa Mashariki mwa DRC.
Habari Picha 10342
Makamu wa Rais amepongeza jitihada mbalimbali zinazoendelea katika kutafuta ufumbuzi wa migogoro katika nchi za ICGLR.
 Jitihada hizo ni pamoja na zinazongozwa na Rais wa Angola, João Lourenço, za kutafuta amani nchini DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati; kusainiwa kwa mkataba wa amani nchini Qatar; kuunganishwa kwa michakato ya Luanda na Nairobi; na mkataba wa amani kati ya Rwanda na DRC uliosainiwa chini ya usimamizi wa Serikali ya Marekani.
Nchimbi amesema licha ya jitihada hizo, bado kuna changamoto za kiusalama katika nchi mbalimbali, hususan DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Sudan Kusini na Jamhuri ya Sudan.
Amehitimisha kwa kusema kuwa njia ya kuelekea amani inahitaji ushirikiano na dhamira ya dhati kutoka nchi zote za ICGLR ili kukabili changamoto zilizosalia kwa ajili ya kujenga ukanda wenye amani, ustawi na himilivu kiuchumi.

You Might Also Like

TARI Yawaalika Wakulima Kujifunza Teknolojia Bora 88 Mkoani Morogoro

Mtanda Akagua Maendeleo Ya Mradi YA Hoteli Ya Nyota Tano Ya NSSF

TANESCO Tunathamini Wadau Wa Maendeleo- Nyamo-Hanga

Masauni: Mapendekezo Ya Kulifanya NEMC Kuwa Mamlaka Yamepokelewa

Mgahawa unaotembea fursa kwa vijana, kutoa huduma ya unywaji wa kahawa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Dkt Samia Awaaapisha Mawaziri, Awaaagiza Kutumia Rasilimali Za Nchi Kupata Fedha
Next Article ADA-TADEA Yamsimamisha Uanachama Mgombea Mwenza, Yajaza Nafasi Zilizo Wazi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?