Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 17

ADA-TADEA Yamsimamisha Uanachama Mgombea Mwenza, Yajaza Nafasi Zilizo Wazi

Na Lucy Lyatuu

KAMATI Kuu ya Chama Cha ADA -TADEA  kimewavua uanachama wanachama wake  kutokana na kukiuka taratibu mbalimbali za chama hicho huku wakijaza nafasi zilizokuwa wazi.

Waliovuliwa uanachama ni pamoja na aliyekuwa mgombea mwenza chama hicho, Ali Makame Issa,  Katibu wa  Baraza la Vijana, Alphonce Mayunga na Katibu  Mkoa wa Mwanza, Deusdedit Tiba.

Katibu Mkuu wa ADA_TADEA, Salehe Msumari amesema hayo  leo Dar es Salaam  wakati akizungumza na vyombo vya habari na kuongeza kuwa  baada ya chama kujaza nafasi za viongozi hao watapeleka taarifa kwa  Msajili wa Vyama vya Siasa.

Amesema wagombea hao wamevuliwa uanachama kwa sababu mbalimbali na kwamba kuanzia sasa matamko ambayo yamekuwa yakitolewa na aliyekuwa mgombea mwenza hayatatambuliwa na chama hicho.

Amesema nafasi ya Makamu Mwenyekiti  Zanzibar imechukuliwa na Ally Mohamed  kutokana na aliyekuwepo  kuhamia chama kingine cha siasa.

 

Amesema pia wamejaza nafasi nyingine Makamu Mwenyekiti Bara, ambaye ameumwa muda mrefu sana na nafasi hiyo kukaimishwa kwa Farida Abdallahna Katibu Mkuu Mwenezi ambaye alihama chama hicho na nafasi yake kuchukuliwa na Mwenyekiti mkoa wa Simiyu, Luhende Kassim,  na nafasi ya Katibu wa Vijana kuchukuliwana Suzan Thomas.

Kuhusu uchaguzi amesema chama hicho hakijapata nafasi yoyote ya uongozi na kwamba Kamati hiyo imekutana kujadili kuona walipokosea na kuwa na mapendekezo ndani ya chama ya nini kitakachofuatwa.

Kuhusu hotuba ya Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati akizindua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Chama hicho, Juma Ali Khatib amesema wanapongeza kwa hotuba nzuri hususani alipotoa msamaha kwa walioshiriki katika vurugu za Oktoba 29, siku ya uchaguzi.

Habari Picha 10346

Amesema pia  Kamati hiyo inapongeza uundwaji wa Wizara maalum ya Vijana ambayo itagusa mambo mengi yanayohusu kundi hilo.

Khatib amewataka pia vijana kuepukana na hamasa zinazosababisha kushiriki  kwenye maandamano kwa kuwa ni eneo lililoitia doa Tanzania .

Habari Picha 10347

 

 

 

 

 

 

Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.