MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wizara Ya Nishati Yaendelea Kutoa Elimu Kuhusu Matumizi Ya Nishati Safi Ya  Kupikia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wizara Ya Nishati Yaendelea Kutoa Elimu Kuhusu Matumizi Ya Nishati Safi Ya  Kupikia
Habari

Wizara Ya Nishati Yaendelea Kutoa Elimu Kuhusu Matumizi Ya Nishati Safi Ya  Kupikia

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya Nishati imeendesha mafunzo ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma

Mafunzo haya ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Nishati katika kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024–2034, ambao unalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe  wanatumia nishati safi ya kupikia.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati,  Anitha Ringia, ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kutambua umuhimu wa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia na kualika wataalam wa Wizara ya Nishati kutoa elimu husika kwa Watumishi wa wizara hiyo.

Habari Picha 9800

Ringia amesisitiza kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia si tu yanachangia kulinda afya za watumiaji, bali pia ni njia muhimu ya kuhifadhi mazingira na kupunguza uchafuzi wa hewa.

“Matumizi yasiyo salama ya nishati ya kupikia yana madhara makubwa kwa afya na mazingira. Kila mtumishi na Mtanzania kwa ujumla anatakiwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutumia nishati safi ya kupikia kwa manufaa ya taifa letu”. Amesema  Ringia

Awali wakati akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Katiba na Sheria,  Mbaraka Stambuli, amesema chimbuko la kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ni juhudi za Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa kinara katika kusisitiza matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira.

“Tunapaswa kutumia fursa ya mafunzo haya kubadilisha maisha yetu ya kila siku majumbani, ili kusaidia nchi kufikia malengo iliyojiwekea katika mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia”. Amesema  Stambuli.

Habari Picha 9801

Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria walioshiriki mafunzo hayo wameeleza kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kuboresha maisha yao na kuchangia katika utunzaji wa mazingira.

Mafunzo hayo pia yalihusisha wataalam kutoka SESCOM na Positive Cooker ambao walitoa elimu kuhusu majiko ya umeme yanayotumia umeme kidogo.

 

You Might Also Like

Rais Samia afurahia SGR

Rais Samia atambua mchango wa NHIF, WCF

SUA Yawafikia Wafugaji Wa Ng’ombe Wa Maziwa Kwa Tiba Mbadala Ya Homa Ya Kiwele

Tanzania, Japan Kushirikiana Ukuzaji Ujuzi Kwa Vijana

Mkuu wa Mkoa akabidhi matrekta kwa wakulima kutoka Pass Leasing

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TEA, UNICEF na Canada waendeleza mageuzi ya elimu Sikonge
Next Article Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo 2030
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Rais Samia Atangaza Baraza Jipya La Mawaziri
Habari November 17, 2025
Vijana Wahimizwa Kuweka Akiba
Habari November 17, 2025
Rais Samia Amwonya Mwigulu Dhidi Ya Vishawishi
Habari November 14, 2025
ICGLR Yajipanga Kujiimarisha Amani Katika Kanda
Habari November 14, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?