MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waziri Mkuu Majaliwa Azungumzia Urushaji Wa Satelite Tanzania
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Waziri Mkuu Majaliwa Azungumzia Urushaji Wa Satelite Tanzania
Habari

Waziri Mkuu Majaliwa Azungumzia Urushaji Wa Satelite Tanzania

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: SERIKALI inaendelea kutekeleza Mpango Mkakati. wa Anga za Juu utakaoiwezesha Tanzania kurusha satelaiti.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mpango mkakati huo ni wa miaka mitano kuanzia 2024/25 hadi 2029/30.
Majaliwa amesema hayo alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA, lililofanyika Dar es Salaam.
Amesema Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT),  imepata mradi wa Utafiti wa kuwezesha urushaji wa satelaiti unaosimamiwa na Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya anga za juu ikishirikiana na Taasisi ya Anga za Juu ya Japan (JAXA).
“Katika eneo hili Maandalizi ya utungwaji wa Sera, Sheria na uridhiwaji wa mikataba ya Kimataifa ya masuala ya anga za juu yanaendelea,” amesema.
Majaliwa ameitaka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iwakusanye vijana wabunifu wenye uwezo wa kubuni teknolojia zenye manufaa kwa Taifa.
“Lakini simamieni hizi tafiti zenye kutoa matokeo na vijana hao waendelee kupewa fursa na kazi hizo ziingie kwa jamii na zianze kutumika,” amesema.
Kwa Upande wake Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa amesema kuwa Serikali imeendelea kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano ambapo kwa mwaka fedha 2023/24 jumla ya urefu wa kilomita 1,592 za mkongo wa taifa zimejengwa na kufika katika wilaya 83.
“Pia umoja wa watoa huduma za mawasiliano wameweza kujenga jumla ya kilomita 2,595 ambazo zinafanya mkongo wa taifa kuwa na kilomita 13,820.
“Wizara imehamisha shughuli zote zinazohusiana na ujenzi wa mkongo wa taifa wa mawasiliano na kituo cha kuhifadhia data (NIDC) kwenda katika Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),” amesema.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrka, Nardos Bekele-Thomas amempongeza Rais Samia  kwa jitihada anazozifanya katika kuhakikisha Tanzania inatumia ukuaji wa sekta ya TEHAMA katika kuchagiza Maendeleo Endelevu nchini.

You Might Also Like

Walimu Wanaofundisha Lugha Ya Kichina Tanzania Wakutana

Ushiriki Wa Tanzania Jukwaa La Dunia Waongeza Fursa Za Kimataifa Kukabiliana Na Maafa-Dk Yonaz

Tuwaombe Rais Samia, Mwinyi – Sheikh Swed

Dkt Biteko Awasili Barbados Kunadi Nishati Safi Kimataifa

Mkandarasi Atakiwa Kukamilisha Mradi Kwa Wakati

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ulega: Miaka 50 ya ILRI imeinufaisha Tanzania 
Next Article Watafiti Mataifa 10 Kujadili ElimuMsingi Nchini
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?