Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: BARAZA la Mitihani la Tanzzania limefuta matokeo yote ya watahiniwa 67 waliobainika kufanya udanganyifu, pamoja na watahiniwa watano walioandika lugha ya matusi katika mtihani wa Kidato cha Nne.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Dkt. Said Mohamed amesema hayo wakaticakitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
Dkt. Mohamed amesema matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (2) (j) cha Sheria ya
Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2) (b) cha Kanuni za Mitihani Mwaka 2016.
Kwa upande mwingine amesema barazahilo imefungia kituo cha P6384 BSL Open School kilichopo mkoa wa Shinyanga kuwa kituo cha Mitihani ya Taifa kutokana na
kuratibu mipango ya udanganyifu.
kuratibu mipango ya udanganyifu.
“Kituo hicho kinafungiwa kwa mujibu wa Kifungu 4(8) cha Kanuni za Mitihani mwaka 2016 hadi hapo Baraza
litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa Mitihani ya Taifa,” amesema.
litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa Mitihani ya Taifa,” amesema.