MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watafiti Mataifa 10 Kujadili ElimuMsingi Nchini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Watafiti Mataifa 10 Kujadili ElimuMsingi Nchini
Habari

Watafiti Mataifa 10 Kujadili ElimuMsingi Nchini

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: WATAFITI zaidi ya 100 kutoka mataifa 10 ulimwenguni wamekutana katika kongamano la Elimu lililoandaliwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuwasilisha na kujadili matokeo ya tafiti zao mbalimbali walizozifanya kuhusiana na elimu msingi na kutoa mapendekezo namna ya kuikuza elimu hiyo nchini.

Akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahera amesema mada zinazowakutanisha watafiti hao ni muhimu, zijadiliwe kwa kina kwani zinaendana na malengo ya sasa ya nchi,

 

Hivyo maarifa yatakayotolewa na mijadala yafikishwe wizarani ili kuona namna bora ya kuweza kuyatumia katika kuboresha juhudi zinazofanyika.

“Kuna mapitio makubwa katika sera na mitaala ya elimu nchini, ambapo elimu msingi inachukuliwa kama nguzo muhimu ya kuandaa watoto kuwa na uwezo wa kuwa na fikra tunduizi, mbunifu na maadili ya Kitanzania. Hivyo, kupitia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, wataalam hawa watawasilisha machapisho yao na kuweza kujadili namna gani bora, elimu msingi inaweza kutekelezwa vizuri,” amesema.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Elifas Bisanda, amesema chuo hicho kimekuwa ni nguzo muhimu katika kuimarisha ubora wa elimu ya msingi nchini kwani kimekuwa kikitoa mafunzo ya stashahada ya elimu ya msingi tangu  2008 ili kukabiliana na upungufu wa walimu katika ngazi hiyo.

“Pia kongamano hili ni sehemu ya Maadhimisho ya 30 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, chuo hiki kimekuwa mbele katika kuendeleza na kuimarisha elimu ya msingi. Baada ya kuanzishwa shule za sekondari nyingi kwenye kata, walimu wenye stashahada walihamishwa kufundisha sekondari hivyo tulianzisha stashahada ya elimu ya msingi na hata walimu waliomaliza stashahada hiyo walibaki kufundisha shule hizo wakiwa na maarifa bora zaidi,” amesema.

 

Dkt. Janeth Kigobe, Mhadhiri Mwandamizi na Katibu wa kongamano hilo la kimataifa, amesema kumekuwa na haja ya kujadili elimu msingi na kuweka mikakati namna ya kushawishi serikali mbalimbali duniani hususani Tanzania namna ya kukuza elimu msingi kwa manufaa makubwa ya maendeleo ya nchi.

Kabla ya kongamano hilo, kulifanyika matembezi ya hisani katika kitongoji cha Kwamfipa mjini Kibaha ambayo yalilenga kuhamasisha umma kuhusiana na umuhimu wa elimu msingi nchini.

Kongamano hilo lenye ujumbe wa “Uboreshaji wa Elimu Msingi kwa Maendeleo Endelevu” linafanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha  mkoani Pwani ambapo wanazuoni kutoka nchi za Uganda, Zambia, Jamaica, Uswisi, Uholanzi, Jamhuri ya Kongo, Nigeria, Kenya, na wenyeji Tanzania Bara na Zanzibar watakutana kwa pamoja kujadili mustakabali wa elimu msingi.

 

You Might Also Like

Profesa Kabudi Atoa Maagizo Mazito Bodi Ya Ithibati Ya Waandishi Wa Habari

Nzega Kujenga Barabara za Lami, Soko la Kisasa ili Kukuza Uchumi

Elimu Ya Dawa Za Kulevya Kutolewa Kwa Wanafunzi

Madini Yaweka Rekodi Makusanyo Ya Maduhuli

Majaliwa Awaagiza Wahandisi Kuzingatia Miiko, Maadili  Ya Taaluma Yao

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Waziri Mkuu Majaliwa Azungumzia Urushaji Wa Satelite Tanzania
Next Article Polisi Yaimarisha Usalama Timu za Simba na Yanga Kesho
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?