MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wachimbaji Wadogo Wafikiwa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wachimbaji Wadogo Wafikiwa
Habari

Wachimbaji Wadogo Wafikiwa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI inaendelea na juhudi za kupunguza mzigo wa tozo kwa Wachimbaji wadogo wa dhahabu hapa nchini kwa kufanya mapitio ya ada na ushuru mbalimbali anazotozwa katika mnyororo wa uchimbaji na uchenjuaji wa madini.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde, amesema hayo  Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Busanda, Tumaini Magessa ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itapitia upya tozo zilizopo kwenye mnyororo wa uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu zinazowaelemea Wachimbaji Wadogo.
Katika majibu yake, Waziri Mavunde amesema kuwa kupitia Mkakati wa Kuboresha Mazingira ya Biashara, Wizara ya Madini imefanya utafiti wa tozo 66 zinazotozwa na Halmashauri mbalimbali katika shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu.
Ametaja tozo hizo kuwa ni ushuru wa karasha, ada ya ukaguzi, kodi ya  thamani, ushuru wa kusafirisha miamba ya madini, na visusi (mabaki ya miamba baada ya uchenjuaji).
“Katika kutatua changamoto hizi, Wizara iliitisha kikao Mwezi Agosti, 2024 Mkoani Singida ambacho kilishirikisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Fedha, Tume ya Madini, STAMICO, Halmashauri za Wilaya (Ikungi, Chunya, Kahama, Msalala, Meatu, Shinyanga, Mtama na Lindi),
“FEMATA na TAWOMA. Rasimu ya Mapendekezo ya Maboresho tayari imeshaandaliwa na ipo katika hatua ya kufanyiwa mapitio na tathmini, ambapo Matokeo ya tathmini hiyo yatatusaidia katika kupanga tozo rafiki kwa wachimbaji wadogo,” amesema.
Pia amesema serikali inaendelea na maboresho makubwa ya mfumo wa kodi kupitia Tume ya Maboresho ya Kodi iliyoanzishwa na  Rais Samia Suluhu Hassan, tume hiyo inatarajiwa kutoa mapendekezo yatakayosaidia kupunguza changamoto za kikodi zinazowakabili wachimbaji hao wadogo.
Hatua hizo zinadhihirisha dhamira ya Serikali katika kuboresha mazingira ya uchimbaji mdogo wa madini na kukuza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi.

You Might Also Like

Watanzania Acheni Kuchanganya Mazao -Jafo

Mongella Atoa Maagizo Maalum Kwa Viongozi CCM

Maabara Ya Mkemia Mkuu Yashauri Wajasiriamali Wa Kemikali

Sirro: Kasulu Itambue Thamani ya Uwekezaji, Itenge Maeneo Rasmi

Hotuba ya Rais Samia Yachochea Miradi Mikubwa ya Viwanda na Bandari Bagamoyo – Mgalu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ushiriki Wa Wanawake, Wasichana Katika Sayansi Ni Mdogo
Next Article Masauni: Mapendekezo Ya Kulifanya NEMC Kuwa Mamlaka Yamepokelewa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Diwani Kata Ya Majengo Awasihi Wananchi Kufanya Kazi Kwa Bidii
Habari February 16, 2026
Tanzania Yalenga Kufikia Asilimia 51 Ya Ushiriki Wa Wanawake Katika Sayansi
Habari February 14, 2026
Makamu wa Rais Asisitiza Ubunifu, Uwekezaji Soko La Hisa La Dar es Salaam
Habari February 13, 2026
JAB Yasisitiza Ithibati Kama Njia ya Kuimarisha Ubora na Uaminifu wa Habari
Habari February 13, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?