MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Trilioni 1.3  Zatumika Kuboresha Afya Ya Msingi Nchini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Trilioni 1.3  Zatumika Kuboresha Afya Ya Msingi Nchini
Habari

Trilioni 1.3  Zatumika Kuboresha Afya Ya Msingi Nchini

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na  Mwandishi Wetu

KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kiasi cha Sh.Trilioni 1.3 kimetumika kufanya maboresho makubwa kwenye miundombinu ya kutolea huduma za afya, vifaa na vifaa tiba, dawa na ubora wa utoaji wa huduma za afya ya msingi nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, Tawala Za  Mikoa Na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Rashid Mfaume ameyasema hayo alipokuwa akizungumzia mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita katika utoaji wa huduma za afya ngazi ya msingi nchini.

Amesema fedha hizo zimetumika kufanya uwekezaji katika afya msingi na kuchangia ongezeko la miundombinu ambapo hadi sasa kuna zahanati 6163, vituo vya afya 932 na hospitali za Wilaya 188.

“Mpaka sasa kuna hospitali mpya za Wilaya 129 ambazo zimejengwa kwenye maeneo ya pembezoni, hospitali kongwe 48 zimeboreshwa, vituo vya kutolea huduma za afya 367 vyenye uwezo wa kufanya upasuaji, kuongeza, damu,” amesema.

Dkt. Mfaume amesema uwekezaji huo umesaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kutoka vizazi hai 556 hadi 104 katika kila vizazi hai 1000.

Pia, amesema katika maeneo ya vijijini kulikuwa na changamoto kubwa ya kupeleka watumishi wa afya na ilitokana na kutokuwa na nyumba za kuishi lakini mpaka sasa Serikali imejenga nyumba 270 kwa ajili yao.

Pamoja na hayo, amesema Serikali imejenga majengo ya kutolea huduma za dharura 86, magari ya kubebea wagonjwa 382 yamesambazwa kwenye halmashauri zote huku kwa kipindi hicho watumishi 25,936 wameajiriwa.

You Might Also Like

SIDO jengeni viwanda 20 Kila mkoa-Jafo

Rais Samia Aongoza Waombolezaji Kutoa Heshima Za Mwisho Kwa Mbunge Ndungulile

Rais Samia azindua bwawa la umwagiliaji Mtibwa

Ridhiwan Kikwete Apongeza Halmashauri Ya Tunduma

Mfumo Uendeshaji Mashauri Kidigitali Kwa Watumishi wa Umma Uharakishwe

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ridhiwani Aiagiza CMA Kushughulikia Migogoro Kwa Haraka, Ufanisi
Next Article Kanisa La GCC Kufanya Maombi Kuelekea Uchaguzi Mkuu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?