Na Lucy Ngowi
ARUSHA: MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA), imesaini hati ya makubaliano katika maeneo ya udhibiti wa viatilifu ili kulinda afya ya walaji pamoja na mazingira.
Pia katika eneo la kuendeleza na kutengeneza miongozo mbalimbali kwa ajili ya udhibiti wa viatilifu , pamoja na kuangalia matumizi ya mifumo ya kimataifa katika kutambua kemikali.mbalimbali pamoja na kuweka vibandiko.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Profesa Joseph alisema TPHPA kwa kushirikiana na Taasisi ya udhibiti wa kemikali ya nchini Sweden(KEM) wamesaini hati hiyo ya makubaliano kwa lengo la kuendeleza mashirikiano ya pamoja katika utendaji kazi zao .
Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini makubalino hayo ofisini kwake.
Profesa Ndunguru alisema, mashirikiano hayo ni mwendelezo kwa kuwa wamekuwa na mashirikiano kati yao na Taasisi hiyo ambapo katika mashirikiano hayo wataalamu kutoka TPHPA wamekuwa wakienda kupata mafunzo nchi ya Sweden ya namna mbalimbali ya kudhibiti matumizi ya viatilifu
Vile vile alisema nao wamekuwa wakija kushirikiana nao pamoja na Taasisi nyingine mbalimbali hapa Tanzania katika kufanya utafiti wa viatilifu hai katika kudhibiti visumbufu mbalimbali vya
“Ushirikiano huu ni mzuri kwani malengo ya mamlaka ni kuleta tija hasa katika kilimo pamoja na kulinda afya ya walaji,wanyama na mazingira kwa kuwa na matumizi sahihi na salama ya viatilifu kwa hiyo hili.ni jambo zuri kwa leo hii kwa kusaini hati hii ya makubaliano pamoja na wenzetu wa Sweden,” alisema.
Alisema kuwa matarajio baada ya kusaini makubaliano hayo ni kuhakikisha tija inaongezeka katika kilimo,na matumizi sahihi ya viatilifu katika kudhibiti visumbufu pamoja na kupungua kwa athari hasi za viatilifu katika mazingira pamoja na kulinda afya ya binadamu na kujengeana uwezo wa watalamu katika tasnia nzima ya matumizi sahihi na salama ya viatilifu nchini.
Alifafanua ili uweze kufanikiwa na kufika mbali lazima mashirikiano yawepo baina ya Taasisi moja na Taasisi nyingine kwani wana maono makubwa ya kutaka kuona taasisi hiyo inakuwa taasisi mahiri ya kudhibiti masuala yote ya afya ya mimea na viatilifu Tanzania.
“”Na ili tuweze kufika hapo lazima tushirikiane na taasisi nyingine kwa kufanya hivyo tunaweza kujipatia rasilimali ya ziada kwa ajili ya kuongeza rasilimali kwani huwezi kutegemea serikali peke yake na hayo ni malengo ya serikali kuhakikisha mashirikiano yanakuwepo.
Kwa upande wake Msimamizi wa mradi kutoka KEM , Raphael Mwezi alisema mashirikiano hayo.yalianza tangu mwaka 2018 ambapo TPHPA pamoja na Taasisi ya Sweden ziliingia kwenye mashirikiano ya kudhibiti sumu ambapo wamefanya mengi ikiwemo kubadilishana uzoefu kupatiana mafunzo na kupeana mbinu za uzoefu kati ya usimamizi wa viatilifu.
‘katika.mashirikiano hayo tuliendelea hadi kufikia mwaka 2023 hadi 2024 ambapo tuliona kuna umuhimu wa kuingia kwenye makubaliano haya mapya.
“Leo katika makubaliano hayo tumekubaliana mambo matatu hayo matatu,” alisema.
Meneja katika kitengo cha usimamizi wa teknolojia ya unyunyuziaji wa viatilifu (TPHPA) Dkt. Magreth Francis alisema, wamefurahi kushirikiana na KEMI kwani moja ya majukumu.yao.katika kitengo wanatamani kuwafundisha wakulima juu ya matumizi sahihi ya viatilifu yenye lengo la kumlinda binadamu, mazingira na kuhakikisha wanapata mazao yaliyo masafi kwa ajili ya soko la nje na la ndani.
Alisema mashirikiano hayo yatakuwa ya muhimu! kwao kama.watapata uwezeshaji kutoka kwao maana watawawezesha kuwafikia wakulima kuwafundisha matumizi sahihi pamoja na upimaji wa afya hasa kwa watumiaji wa viatilifu na kupata majibu mazuri namna sahihi ya matumizi ya viatilifu.