MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TIRA Yasisitiza Umuhimu wa Bima katika Kulinda Uchumi wa Taifa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TIRA Yasisitiza Umuhimu wa Bima katika Kulinda Uchumi wa Taifa
Habari

TIRA Yasisitiza Umuhimu wa Bima katika Kulinda Uchumi wa Taifa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
TANGA: bAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imesisitiza kuwa bima ni nyenzo muhimu ya kulinda maisha ya wananchi na uchumi wa taifa, na si jambo la hiari kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidhani.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea mkoani Tanga kuanzia Januari 19 haLupilyamwaka huu 2026, Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini, Dkt. Emmanuel Lupilya, amesema bima ina mchango mkubwa katika kulinda shughuli za kilimo,
Biashara na uzalishaji, pamoja na kupunguza athari za majanga kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa baada ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dadi Kolimba, kutembelea banda la TIRA katika maadhimisho hayo.
Dkt. Lupilya amesema TIRA haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya makampuni ya bima yatakayokiuka miongozo, sheria na taratibu zilizowekwa, akisisitiza kuwa ukiukwaji wa sheria hizo unakwamisha ukuaji wa sekta ya bima na maendeleo ya uchumi wa taifa.
Ameeleza kuwa mamlaka hiyo, kwa kushirikiana na makampuni ya bima, inaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza uelewa wa masuala ya bima, akibainisha kuwa ukosefu wa elimu hiyo hulazimisha serikali kubeba mzigo mkubwa wa kifedha unaotokana na majanga, umaskini na mdororo wa uchumi.
“Endapo taifa halitaelimishwa kuhusu umuhimu wa bima, serikali italazimika kugharamia athari za majanga, umaskini na kushuka kwa shughuli za uzalishaji, hali inayoliletea taifa mzigo mkubwa wa kiuchumi,” amesema.
Ameongeza kuwa juhudi za TIRA na makampuni ya bima katika kutoa elimu kwa umma ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha ukuaji wa pato la taifa na kuimarisha ustawi wa wananchi.
Sambamba na hilo, amezitaka kampuni za bima kuwa wabunifu katika kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji halisi ya wananchi, badala ya kuangazia zaidi maslahi ya makampuni yenyewe.

You Might Also Like

Taasisi Za Umma Zasisitizwa Kuzingatia ubora Wa Mikataba Katika Utekelezaji Wa Majukumu Yao

UDSM Yapiga Hatua Kubwa Kuboresha Miundombinu na Mitaala kwa Mradi wa HEET

Dkt. Mashimba Achukua Fomu Ya Kuwania Nafasi Ya Ubunge

Majaliwa Amwakilisha Rais Samia Kwenye Kilele Cha Siku Ya Utumishi Wa Umma

Watafiti Wa Mimea Vamizi Watua Serengeti

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wiki ya Huduma za Fedha: SELF Yafungua Fursa za Kiuchumi kwa Wananchi Tanga
Next Article Uwekezaji wa TIB Wachangia Kuongezeka kwa Ajira
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TTCL  Yatumia Tamasha La Kizimkazi Kueleza  Wananchi Fursa Wanazotoa
Makala August 15, 2026
Rais Samia Afurahishwa Na Huduma za NSSF
Habari August 13, 2026
  VETA Yashiriki Tamasha La Kizimkazi
Habari August 13, 2026
Vijana Watakiwa Kuanza Utekelezaji Wa Mipango Waliyonayo
Habari August 12, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?