Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA Dkt. Erasmus Kipesha akisisitiza jambo katika kikao cha tano kilichofanyika mjini Morogoro Septemba 11 na 12, 2025. Kulia ni Katibu msaidizi Lusungu Kaduma
Na Mwandishi Wetu
MOROGORO: MKURUGENZI Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha, ameeleza kuwa Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu linalowawezesha watumishi kushiriki moja kwa moja katika upangaji wa mipango na utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
Dkt. Kipesha ameeleza hayo katika kikao cha siku mbili cha Baraza la Wafanyakazi cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Mamlaka kwa mwaka wa fedha 2024/2025, pamoja na kuwasilisha na kuchambua mpango kazi wa mwaka 2025/2026.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA Dkt. Erasmus Kipesha (kulia) pamoja na Katibu wa Baraza hilo Mwanaisha Komba (kushoto) wakifuatilia taarifa na maoni kutoka kwa wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha tano kilichofanyika Morogoro
Amesema ushiriki wa watumishi katika kujadili utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka na mikakati iliyowekwa kwenye utekelezaji ni msingi wa uwajibikaji, ufanisi na mafanikio ya taasisi kwa ujumla.
“Mkutano huu ni fursa mahsusi ya kujitathmini, kubadilishana mawazo, na kupanga kwa pamoja mikakati ya kuimarisha utendaji wetu ili kufanikisha malengo ya Mamlaka,” amesema Dkt. Kipesha.

Kaimu Mkurugenzi Utafutataji Rasilimali na Usimamizi Miradi ya Elimu Masozi Nyirenda akitoa ufanunuzi kuhusu utekelezaji wa miradi ya elimu kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA mjini Morogoro
Katika kikao hicho, wajumbe wamepata fursa ya kupokea taarifa za utekelezaji kutoka kwa vitengo mbalimbali vya Mamlaka, na kutoa maoni na mapendekezo ya namna ya kuboresha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi zaidi.

Wajumbe wa Baraza la Pili la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana kwenye kikao cha tano cha baraza hilo Morogoro.