Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: BUNGE lipo tayari kuishauri serikali kwenye eneo la kisera ambalo halijakaa sawa ili lifanyiwe maboresho.
Aidha kwa upande wa sheria bunge lipo tayari kuibadili ili nchi iweze kupiga hatua.
Spika wa Bunge Tulia Ackson amesema hayo wakati akifungua Kongamano la Uhuru wa Wana Taaluma katika Afrika linalofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema,” Lazima wanataaluma kila mmoja kwenye taaluma yake, mawazo wanayoyafikiria watuletee ili kwenye jamii yetu tuweze kusonga mbele, tuweze kupiga hatua,”.
Amesema wanataaluma hao watapata nafasi ya kujadili uhuru wa kusema mawazo yao kwa sababu wao ni watu wa utafiti, kujaribu kusema ule utafiti walioufanya na mambo ambayo wanatarajia kufanya kwenye jamii.

.
” Zile changamoto walizosema wanataaluma hawa, mojawapo ni kuangalia namna ya wanavyoweza kuingiliwa na wanasiasa lakini viongozi wa kiserikali,
” Uhuru wa wanataaluma usiwe unaingiliwa na serikali, wana siasa hata wao kwa wao wameweza kufanya kazi kwa uhuru. Hata wao sasa hivi wanakiri umevuka mipaka ya kujadili na kusema,” amesema.

Amekiri kuwa watu wanaofundisha vyuo vikuu wana uwezo wa kufikiri, kuwa na mawazo mapya na ndio maana wanabakishwa vyuo vikuu.
“Ni watu ambao wana akili nyingi tuseme ule uhalisia,” amesema.
Naye Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii UDSM, Profesa Christine Noe amesema mkutano huo wanarejea makubaliano waliyokubaliana kwa kuwa wanaona taaluma na wanataaluma sauti zao zimepotea na jamii inaona kuna umbwe wanataaluma hawapo tena.
Profesa Noe amesema, ” Jamii haisikii matukio makubwa yanayoendelea, taaluma na wana taaluma hawasemi kwa sauti zinazosikika wakati huo tunafanya tafiti sana, tunaandika machapisho mengi lakini jamii inakosa ile taaluma,

“Viongozi nao wanakosa kujua kile tunachokifanya , tunajitathmini kazi yetu inakuja, sauti zetu hazisikiki, matokeo ya kazi yetu hayaendi mbali,” amesema.
Kongamano hilo limeanza leo Aprili 29 hadi Mei 2, 2025 limeandaliwa na Ndaki ya Sayansi za Jamii UDSM kwa ushirikiano na Kanseli ya Maendeleo ya Utafiti katika Sayansi za Jamii (CODESRIA).