MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Sera mpya ya biashara irahisishe ufanyaji biashara
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Sera mpya ya biashara irahisishe ufanyaji biashara
Habari

Sera mpya ya biashara irahisishe ufanyaji biashara

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu
NAIBU  Waziri Mkuu, na Waziri wa Nishati  Dkt. Doto Biteko, amezindua Sera mpya ya taifa ya biashara na kubainisha mambo matano ambayo ni pamoja na sera hiyo  kuimarisha uwezeshaji na kurahisisha mazingira ya ufanyaji biashara.
Aidha ametaka itumike kuongeza thamani ya bidhaa za ndani na kuongeza ushindani wa mauzo ya bidhaa za Tanzania  na nchi za nje.
Dkt. Biteko amesema hayo Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Sera hiyo, hafla ambayo ilihudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali,  mawaziri, naibu  mawaziri na makatibu wakuu pamoja na wadau mbalimbali wa biashara.
Amesema kuna umuhimu wa kutumia Sera hiyo kuondoa vikwazo vya biashara na kuweka mfumo wa sheria unaolenga kuimarisha na kukuza biashara na kuwataka maofisa wa serikali kuachana na tabia ya kukwamisha mambo.
“Tuunge mkono ndoto za kiongozi wetu Rais Samia na asiwepo wa kukwamisha utekelezaji wa sera hivyo na pindi ikitokea hatosita kuchukua hatua,” amesema Dkt Biteko na kuongeza kuwa  Waziri wa Wizara husika  ajue kuwa atapatà mapingamizi  mengi kwa baadhi ya watu lakini atamsaidia.
Amesema hakuna faida ya kuwa na Sera nzuri lakini wakawepo maofisa ambao kazi yao ni kukwamisha wafanyabaishara na aliwataka kutumia sera kuwa kiunganishi baina ya wafanyabiashara na serikali.
Amesema Sera ni  nyaraka na isiposimamiwa  itabakia kuwa kitabu Cha hadithi  kwa hiyo ni muhimu  kubadilisha mtazamo na fikra  Ili kuwa wazuri  kwenye kuandika na kuyafanyia kazi pia.
 Amewataka wafanyabiashara wote nchini kufahamu kuwa serikali ni yao na kwamba inapenda kuona wananufaika na biashara wanazofanya huku akiwaonya wenye tabia ya kukwepa kodi.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara,  Dkt Selemani Jafo amesema sera hiyo imewezekana kutokana na msaada wa wadau mbalimbali zikiwemo balozi za nchi mbalimbali na kampuni ya  Trade Mark Afrika.
“Wadau wengi sana wamehusishwa lengo likiwa ni   kuhakikisha tunapata Sera inayoakisi hali halisi ya sasa, nawapongeza wataalamu wa wizara yangu wamefanyakazi usiku na mchana na kupitia sera hii tunatarajia kuongeza sana mauzo ya nje ikiwemo masoko ya Afrika,” amesema.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta binafsi (TPSF) ,Rafael Maganga amesema wamekuwa wakipigia kelele muda mrefu, kwa hatua hiyo Sekta binafsi imefurahishwa
Itasimamia masuala  ya Biashara Kwa urahisi zaidi.

You Might Also Like

Waajiri Wathamini Taaluma Ya Uandishi Wa Habari – Dkt. Mkoko

Wagonjwa 472 Waonwa Na Daktari Wa Mifupa MOI, 40 Wapendekezwa Kufika Dar kwa Matibabu

Serikali Kumuenzi Mzee Morris, Ngoma Zake 10

Wanafunzi Wawili Wajiteka Ili Wapate Pesa Toka Kwa Wazazi wao

Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Samia kufanya ziara mkoani Morogoro, kuzindua safari za SGR
Next Article Rais Samia katika uzinduzi rasmi safari za SGR
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?