MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ridhiwani: WCF Umeboresha Mifumo Ya Ushughulikiaji Wa Fidia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ridhiwani: WCF Umeboresha Mifumo Ya Ushughulikiaji Wa Fidia
Habari

Ridhiwani: WCF Umeboresha Mifumo Ya Ushughulikiaji Wa Fidia

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
DODOMA: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amesema serikali inaendelea kutekeleza dhamira ya kuwalinda wafanyakazi ambao ni nguzo muhimu katika maendeleo ya Nchi.
Ridhiwani amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),  tangu kuanzishwa kwakwe, ikiwa ni hatua kubwa katika kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na familia zao.
Amesema WCF imeongeza wigo wa mafao ambapo hadi sasa unatoa jumla ya mafao saba ikiwemo Fao la Matibabu yasiyo na kikomo, Fao la Ulemavu wa Muda Mfupi, Fao la Ulemavu wa Kudumu, Fao la pensheni kwa wategemezi, Fao la Wasaidizi wa Mgonjwa, Fao la Utengamao na Fao la Msaada wa Mazishi.
Amesema WCF umeboresha mifumo ya ushughulikiaji wa fidia kwa wafanyakazi kwa kutumia mifumo ya TEHAMA ambapo hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya huduma zinazotolewa zinapatikana mtandaoni, hali ambayo imeongeza ufanisi na tija katika utendaji kazi wa mfuko.
Pia amesema mfuko huo umekuwa ukitoa elimu na uhamasishaji kwa waajiri na wafanyakazi kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi na usalama kazini, hivyo wafanyakazi wengi kuelewa haki zao pale wanapopata ugonjwa ama ajali zinazotokana na kazi zao.
Kwa upande mwingine Waziri Ridhiwani amesaini kanuni zinazoanzisha fao jipya la Utengamao linalolenga kumsaidia kumrudisha mfanyakazi aliyeumia kazini katika hali ya kuweza kuzalisha na kuendeleza msingi bora wa maisha.
Ridhiwani ameishukuru menejimenti  ya WCF kwa kuishi maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwahakikishia watanzania  kuendelea na uzalishaji hata baada ya kuumia kazini.
Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma amesema mfuko huo umepewa cheti cha ithibati katika utoaji wa huduma bora kwa viwango vya Kimataifa Juni mwaka jana, 2024 hatua inayoongeza imani chanya kwa wadau wote wanaohusika kwenye mnyororo wa fidia kwa wafanyakazi nchini.

You Might Also Like

Mafunzo Yatolewa Katika Kongamano La Jotoardhi

BoT: Tumia Taasisi za Fedha Halali kwa Usalama wa Kifedha

Wataalamu wa Tanzania, Kenya Watoa Ufafanuzi Kuhusu Maana Na Matarajio Ya Jumuiya Ya China, Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja

JOWUTA Yataka Sheria Za Kazi Kuwalinda Wafanyakazi Katika Vyombo Vya Habari

Mpango Asema Tanzania, Korea Kubadilishana Wafanyakazi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article MOI Yaokoa Bilioni 150 Matibabu Ya Kibingwa
Next Article MOI Yaeleza Sababu Viungo Bandia Kuuzwa Kwa Bei Kubwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Yaingia Makubaliano Ya Ushirikiano Na DIT Kuimarisha Usimamizi Wa Mataifa
Habari June 8, 2026
Wananchi Waelimishwa Masharti ya Kubadilisha Noti Zilizochakaa, Kuungua na Kuchanika
Habari June 7, 2026
DMI Yawaalika Vijana Kujiunga Na Masomo Ya Ubaharia
Habari June 6, 2026
Taifa Gas Yaendelea Kuongoza Kampeni ya Nishati Safi kwa Taasisi na Sekta ya Utalii Tanzania
Habari June 6, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?