MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ridhiwani Kikwete Atembelea Banda la REA, Aipongeza Kasi ya Usambazaji Umeme Vijijini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ridhiwani Kikwete Atembelea Banda la REA, Aipongeza Kasi ya Usambazaji Umeme Vijijini
Habari

Ridhiwani Kikwete Atembelea Banda la REA, Aipongeza Kasi ya Usambazaji Umeme Vijijini

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, ametembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kujionea utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme pamoja na matumizi ya mifumo ya kidigitali inayorahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wananchi.
Akiwa katika banda hilo, Ridhiwani amepata maelezo kutoka kwa Ofisa Upimaji Mwandamizi wa REA, Hussein Shamba, aliyemueleza maendeleo ya usambazaji wa umeme katika vitongoji nchini na mafanikio ya matumizi ya mfumo wa kidigitali wa ufuatiliaji wa miradi hiyo.
Habari Picha 12387
Shamba amesema kasi ya usambazaji wa umeme vijijini imefikia asilimia 77, ambapo jumla ya vitongoji 39,840 tayari vimefikiwa na huduma ya umeme.
Amebainisha kuwa vitongoji 12,736 vilivyobaki vinatarajiwa kukamilishwa ifikapo mwaka 2030/2031.
“Kwa sasa tupo katika hatua ya juu ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, na tunatarajia kukamilisha vitongoji vyote vilivyobaki ndani ya muda uliopangwa,” amesema Shamba.
Aidha, amefafanua kuhusu mfumo wa kidigitali unaowawezesha wananchi kupata taarifa mbalimbali za huduma ya umeme kupitia simu zao za mkononi, ikiwa ni pamoja na hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo yao.
Amemwonesha Waziri mfano wa Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo, Jimbo la Chalinze, ambapo mfumo huo umeonyesha kuwa vijiji 286 vina umeme, vijiji 133 vipo kwenye mpango wa utekelezaji, huku vitongoji 50 vikiwa katika hatua ya utekelezaji wa wakandarasi waliopo maeneo ya kazi.
Mfumo huo pia unaonesha kwa uwazi vitongoji vyote vilivyofikiwa na umeme pamoja na vile vilivyo kwenye mpango wa kufikishiwa huduma hiyo, hatua inayolenga kuongeza uwazi na ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.
Katika hatua nyingine, Ridhiwani ameoneshwa matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambapo alikabidhiwa jiko la sahani mbili kwa ajili ya kuendelea kutoa hamasa na kuwa mfano katika matumizi ya nishati hiyo katika jamii mbalimbali nchini.

You Might Also Like

RAAWU na mafanikio iliyopata utawala wa Rais Samia

Programu Ya Samia Extended Scholarship Yazinduliwa

Mjadala na Kampuni za Nishati Kimataifa Kuendelezwa

Umwagiliaji kumwezesha mkulima kulima mara mbili mpaka tatu kwa mwaka

TEA, Wadau Kuwezesha Matumizi Safi Nishati Ya Kupikia Mashuleni

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ridhiwani Aipongeza TEA kwa Kuimarisha Elimu Nchini
Next Article  Mfumo Wa REA  Wa Digital Platform  Wapongezwa Na Waziri Kikwete
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

SmartDarasa: Tunda la Miaka 40 ya COSTECH Linalobadili Elimu ya Sayansi Tanzania
Makala August 1, 2026
TVLA Yazalisha Chanjo ya Kudhibiti Homa ya Kutupa Mimba kwa Mifugo
Habari August 1, 2026
Halmashauri Ya Jiji La Dodoma Lawataka Wakulima Kutumia Nanenane Kujifunza Kilimo Cha Kisasa
Habari August 1, 2026
Dkt. Nchemba: TPHPA Yazidi Kuwafikia Wakulima
Habari August 1, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?