MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ridhiwani Aongoza Waliojiajiri Kujiunga, Kuweka Akiba NSSF
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ridhiwani Aongoza Waliojiajiri Kujiunga, Kuweka Akiba NSSF
Habari

Ridhiwani Aongoza Waliojiajiri Kujiunga, Kuweka Akiba NSSF

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

PWANI: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amepongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kuanzisha Skimu ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii kwa Wananchi Waliojiajiri yenye jina la kampeni “NSSF STAA WA MCHEZO”.

Ridhiwani ametoa pongezi hizo alipowaongoza wananchi wa Chalinze mkoani Pwani, katika muendelezo wa elimu kwa umma kuhusu skimu hiyo.

Ametoa pongezi hizo kwa kuwa skimu hiyo itakuwa mkombozi kwa wananchi waliojiajiri ili kunufaika na mafao ya muda mfupi yakiwemo ya matibabu na mafao ya muda mrefu ambayo ni uzeeni.

Hivyo Ridhiwani amewaelekeza wananchi waendelee kujiunga na kujiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya sasa na ya baadaye.

“Unapojiunga na skimu hii pale unapougua utanufaika na matibabu, ukipata ulemavu utanufaika na mafao ya ulemavu, ukiwa mzee utanufaika na mafao ya uzeeni hivyo ni muhimu kila mwananchi kuchangamkia fursa hii, kwa kujiweka akiba,” amesema.

Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maoni na miongozo yake ambapo kupitia serikali wananchi waliojiajiri wanajiwekea akiba NSSF na kunufaika na mafao na huduma nyingine.

“Mpango ulioletwa na NSSF ni kwa ajili ya leo na kesho yako, kwani itafika siku nguvu ya kufanyakazi zitapungua na hapo ndipo NSSF itachukua nafasi ya kuwa Staa wa Mchezo kwa kulipa mafao ya pensheni ya uzee na matibabu,” amesema.

Amesema NSSF imeweka utaratibu nzuri wa kujiunga na kuchangia kidogo kidogo kwa siku buku buku, hivyo amewataka wananchi kuendelea kujiunga na kuchangia ili kunufaika na mafao pamoja na huduma nyingine zinazotolewa na Mfuko.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Omary Mziya amesema hifadhi skimu inawahusu wananchi waliojiajiri katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi,

Na kwamba itafungua milango kwa wananchi kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa na NSSF yakiwemo matibabu.

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Hassan Mwinyikondo ameipongeza NSSF kwa kuja na skimu hiyo ambayo itakuwa mkombozi kwa wananchi waliojiajiri.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga amemewahakikishia wananchi wa Chalinze na Bagamoyo kuwa mpango huo ni mkombozi kwa wananchi hususani watakapoishiwa nguvu ya kufanyakazi, kwani watapata mafao kutoka NSSF.

You Might Also Like

PSSSF MSHINDI WA KWANZA TUZO ZA UANDAAJI BORA MAHESABU ZA NBAA, 2023

Mwanjala Wa TRC Aelezea Umuhimu Wa VETA

Kongamano  La Kimataifa La Jotoardhi Laanza Kwa Mafanikio

Mawakili Wa Serikali Watakiwa Kuzingatia Katiba Ya Nchi Wanapoandika Sheria

Zifahamu hifadhi za bahari na maeneo tengefu.

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article NCCR-MAGEUZI Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 
Next Article TEA, Wadau Kuwezesha Matumizi Safi Nishati Ya Kupikia Mashuleni
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?