Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwan Kikwete amefanya mazungumzo na Waziri anayeshughulikia masuala ya kazi na ajira wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Balozi AbdulrahmanAl Awar.
Ridhiwan amesema akiwa na Waziri huyo, wameweka mikakati ya ukuzaji Kaz, Ajira na utekelezaji wa Makubaliano hayo baina ya Tanzania na UAE.
