Na Lucy Lyatuu
MGOMBEA  Ubunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Profesa Kitila  Mkumbo amesema watanzania wanayo kila sababu ya kumchagua mgombea Urais anayetokana na CCM  Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa alizofanya katika awamu yake ya kwanza ikiwemo kuwahakikishia watanzania amani, usalama na Utulivu.

Akizindua kampeni katika Jimbo la Ubungo leo septemba  06,2025 Profesa Kitila amesema ndani ya kipindi cha miaka minne na nusu aliyoongoza Rais Dkt  Samia Tanzania imeshuhudiwa ikiendelea kuwa Nchi yenye Amani zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika ya Kati.

Amesema pia Dk. Samia ametekeleza kikamilifu Ilani ya CCM kwa kujenga miundombunu ya barabara, reli, madaraja na kukuza biashara na uwekezaji.





