Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 16

NFRA Yafundisha  Wakulima Mbinu Za Kuhifadhi Mazao

Na Lucy Lyatuu,Tanga

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi Ya Chakula (NFRA)  inaelimisha jamii mbinu mbalimbali za uhifadhi wa  chakula ili wakulima waweze kutunza chakula kwa njia zilizo bora pamoja na kukabiliana na mvua za Elnino.

Aidha Wakala umesema  ipo njia ya asili ya kutambua mazao yaliyokauka  ili yaweze kuhifadhiwa ikiwa ni pamoja na kuweka mazao hayo  kwenye chupa kavu ya plastiki na kuchanganya na chumvi kisha kuifunga na inaweza kutoa  matokeo baada ya dakika tano.
Habari Picha 14073
Ofisa Kilimo kuyoka NFRA Mathay Hhando amesema hayo katika siku ya chakula duniani inayoadgimishwa mkoani Tanga katika viwanja vya Usagara.

Amesema NFRA inawafundisha wakulima kuhifadhi chakula kwa mbinu bora ili kisiharibike na kuwa salama kwa matumizi.

Amesema mkulima anaweza kuhifadhi chakula kwenye mifuko maalum lakini sharti isiwekwe kugusana na sakafu ama ukuta wa nyumba,jambo litakalowezesha mazao kukaa kwa  muda mrefu huku akiepuka pia kutumia  viuatilifu kuhifadhi mazao.
Habari Picha 14074
“Matumizi ya viuatilifu ni gharama na kwa kutumia njia ya asili mkulima anaweza pia kuhifadhi  mazao katika kihenge cha bati maalum pale ambapo mazao yanakuwa yamekauka,” amesema.
Kuhusu matumizi ya chumvi na chupa amesema mkulima ataweka robo ya mazao hayo kwenye chupa ya plastiki ambayo ni kavu na kuchanganya  na vijiko viwili vya  chumvi na kuweka chupa hiyo kwenye kivuli na baadabya dakika tano kama chumvi ndani ya  chupa itaonesha kuyeyuka ni wazi kuwa mazao hayajakauka ipasavyo.
Amesema iwapo chumvi haitoyeyuka na kubakia kama ilivyo basi mazao hayo yanakuwanyamekauka na yanahitaji kuhifadhiwa.
Habari Picha 14075
“Zipo njia nyingine za kujua kama mazao yamekauka ikiwa ni pamoja na kung’ata punje,kusikiliza mlio wa mazao kwa kumimina kwenye vyombo,” amesema na kuongeza kuwa njia nyingine ya kisasa ninkutumia madhine maalum yankupima unyevu kwenye mazao.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.