Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 11

NAESA Imejiandaa Kutoa Elimu Kwa Wakulima Kutafsiri Taarifa Za  Mvua  Za El Nino

Na Lucy Lyatuu,Tanga

WAKALA Ya Taifa Ya Huduma Za Ugani (NAESA) umesema umejiandaa kutoa elimu kwa wakulima na maofisa ugani kwa  mikoa 14 inayopata mvua mara mbili kwa mwaka  kuhusu namna nzuri ya kutafsiri taarifa za hali ya hewa  kuelekea katika mvua za Elnino.
Kaimu Meneja wa Masoko wa NAESA Ester Mwaisango amesema hayo katika wiki ya chakula duniani inayoadhimishwa mkoani Tanga  katika viwanja vya Usagara.
Amesema NAESA imejiandaa kutoa mafunzo hayo na kwamba inaendelea na majukumunyame ya kusajili wakulima ambapo tayari imewafikia wapatao 5000.
Amesema usajili huo unaendelea na lengo kubwa kuwafundisha namna ya kutumia teknolojia mbalimbali za kuongeza thamani katika mazao.
Habari Picha 14068
Amesema kupitia  maadhimisho hayo NAESA imeshirikisha vyuo vya kilimo wakifundisha wakulima namna ya kuongeza thamani kwenye mazao.
Kwa upande wake Mkufunzi kutoka Chuo Cha Kilimo Ilonga,Hamis Abdallah amesema kupitia maadhikisho hayo NAESA inafundisha wakulima   teknolojia ya kuweka mchele joto ambayo inasaidia kuhifadhi zao hilo kwa muda mrefu bila kuharibika.
Amesema kupitia teknolojia hiuo mkulima anaanza hatua kwa hatua ikiwemo kuchakata mpunga kwa kusafisha ,kutoa mafuta  ndani ya mchele ili uweze kukaa sokoni muda mrefu  lakininpia ukiwa umenyooka bila kukatikakatika.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.