Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 14

Mikoa Inayozalisha Chakula Kwa Wingi Inaongoza Kwa Udumavu.

Na Lucy Lyatuu,Tanga

ŴIZARA ya Afya,Idara Za Kinga na Lishe imesema  mikoa inayozalisha chakula kwa wingi ndio ambayo inaongoza kwa udumavu nchini jambo ambalo linafanyiwa kazi ili kujua sababu  zake.
Imesema  mkoa wa Iringa unaongoza kwa asilimia 56 na Njombe kwa asilimia 54 ambapo serikali inatafuta kujua kiini cha tatizo.
Ofisa Lishe Mwandamizi kutoka Wizara Ya Afya Idara ya Kinga Na Lishe Peter Kaja amesema hayo katika  wiki ya chakula duniani ambayo inaadhimishwa mkoani Tanga katika viwanja vya Usagara.
Amesema  udumavu ni kipimo cha urefu  na umri ambapo  watoto wote  chini ya miaka mitano ni lazima walingane kwa kila kitu na kwamba  anayekuwa tofauti  huingia kwenye taarifa za udumavu.
Amesema watoto huanza kuzidiana baada ya miaka mitano ambapo kila mmoja huchukua maumbile   ya  wazazi ama ndugu husika,hivyo katika malezi na.makuzi ya mtoto siku 1000 za mwanzo zinatakiwa uwekezaji mkubwa ili kuepuka udumavu.
Habari Picha 14084
Amesema kitaifa kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2022 hali ya udumavu ipo kwa asilimia 30 na kwamba jambo linaloshangaza ninkwa mikoa yenye vhakula kuwa na udumavu.
Hata hivyo amesema wazazi wengi hupata watoto bila kujiandaa wengi wakiwa kama wanashtukiza jambo linalosababisha watoto kuzaliwa bila kuwa na madini na vitamin mbalimbali  jambo ambalo linaweza kutishia kuwa na nguvu kazi yenye tija kwa kizazi kijacho.
Amesema serikali kwa kuliona hilo imeongeza biturubishonkwa mazao ya aina nne nchiji ambayo ji unga wa ugali,mafuta ya Kula,chumvi na unga wa  ngano.
Amesema madini hayo ni pamoja  folic asid, vitamin B 12,madini chuma na zink lengo kuwezesha wananchi kuzalisha watoto wenye nguvu inayostahili  kwa kizazi kijacho.
Kwa upande wake  Ofisa Lishe kutoka mkoa wa Tanga,Sakina Mustafa amesema  wanatumia banda la wizara ya afya  kutoa elimu kwanumma kuhusu vyakula vilivyoongezwa virutubishi ili kupunguza tatizo la  udumavu na ukondefu  kwa watoto nchini.
Amesema mkoa huo kuna udumavu kwa asilimia 24.1 ambao huanzia tangu mimba kutungwa mpaka mtoto anapofkkia umri wa miaka miwili hadi mitano iwapo hali yake ya lishe haitokuwa vizuri.
Amesema tatizonla uzitonkupjngua liko kwa asilimia 11.2 na ukondefu kwa asilimia 5.6 ambapo mazao hayo yameongezwa virutubishi  kama madini ya chuma,zink vitamin B 12 na Vitamin B9 jambo linalosaidia wanawake wengi aanaojifungua wakiwa na matatizo ya ukosefu wa madininna vitamini na kulinda watoto wanaozaliwa.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.