MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo 2030
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo 2030
Habari

Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo 2030

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI  imeeleza mafanikio makubwa ya utekelezaji  wa miradi ya kusambaza umeme maeneo ya vijijini  na pembezoni mwa miji ambapo  kupitia Wakala wa Nishati Vijijini  (REA) imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme kwenye vijiji vyote 12,318.

Hatua hiyo ni sawa na asilimia 100 ya miradi ya umeme kwenye vitongoji inatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2030.

Mafanikio ya miradi ya umeme Vijijini  yamebainishwa leo Oktoba 8, 2025 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Umeme Vijijini  Jones Olotu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja jijini Dodoma.

“Tanzania bara tuna jumla ya vitongoji 64,359 ambapo kati ya hivyo vitongoji  37,328 sawa na asilimia 58 vimeshafikiwa na huduma ya umeme na bado miradi ya kusambaza na kufikisha huduma ya umeme inaendelea katika maeneo mbalimbali nchini,” Amesema Olotu.

Halikadhalika, Olotu ameongeza kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini unatarajia kukamilisha utekelezaji wa kusambaza umeme kwenye maeneo ya vitongoji ifikapo mwaka 2030 ili watanzania wapate huduma ya umeme ili kukuza maendeleo yao binafsi na uchumi wa Taifa.

Katika hatua nyingine,  Olotu amesema Serikali imepata watoa huduma kwa ajili ya kufungwa mifumo ya umeme jua kwa wakazi wa maeneo ya visiwani Tanzania bara ipatayo 20,000.

Katika hatua nyingine,  Olotu amewaasa wananchi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali kupitia REA hususan nishati safi ya kupikia kwa ajili ya kujikinga na madhara ya kiafya,  kimazingira na kiuchumi yanayotokana na matumizi ya nishati isiyo safi na salama.

Vilevile, Serikali kupitia REA inaendelea kuwezesha ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta maeneo ya vijijini ili wananchi waweze kuhifadhi salama bidhaa za mafuta.

Watumishi wa REA wameipamba Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo inafanyika katika ofisi ya Wakala wa Nishati Vijijini makao Makuu jijini Dodoma.

 

You Might Also Like

JUMIKITA Yaiomba Serikali Mikopo Ya Fedha, Vifaa

Rais Mwinyi Kuzindua Maabara Nguvu Za Atomi

Tuwaombe Rais Samia, Mwinyi – Sheikh Swed

Ajira kwa Vijana na Afya kwa Wazee: Ajenda Kuu za Wagombea Jimbo la Dodoma Mjini

Kabudi Aelezea Mafanikio Ya Wizara Yake

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wizara Ya Nishati Yaendelea Kutoa Elimu Kuhusu Matumizi Ya Nishati Safi Ya  Kupikia
Next Article Asisitiza Umuhimu Wa Kukamilisha Miradi Kwa Mujibu Kuzingatia Mikataba
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe
Habari October 17, 2025
Mgombea NCCR-Mageuzi Awaasa Watanzania Wasikubali Propaganda
Habari October 17, 2025
Profesa Nombo: Ushirikiano wa VETA, Sekta Binafsi Waimarisha Mafunzo ya Ufundi Stadi
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?