MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mbunge Aibana Serikali Kuhusu Malipo ya Wafanyakazi wa Zamani SPM Mgololo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mbunge Aibana Serikali Kuhusu Malipo ya Wafanyakazi wa Zamani SPM Mgololo
Habari

Mbunge Aibana Serikali Kuhusu Malipo ya Wafanyakazi wa Zamani SPM Mgololo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Mafinga Mjini, Dickson Lutevele, ameihoji serikali kuhusu kuchelewa kwa malipo ya madai ya wafanyakazi wa zamani wa Kiwanda cha Karatasi cha SPM Mgololo, akisema wamekaa muda mrefu wakisubiri haki yao bila mafanikio.
Akiuliza swali la msingi bungeni jijini Dodoma, Lutevele ametaka kufahamu ni lini serikali itatekeleza malipo hayo, akibainisha kuwa kuchelewa huko kumeendelea kuwaathiri wahusika kiuchumi na kijamii.
Katika swali la nyongeza, mbunge huyo amesema wafanyakazi hao walishinda kesi mwaka 2007 ambapo mahakama iliamuru walipwe na pande zote mbili serikali na mwekezaji lakini hadi sasa hawajalipwa.
Amehoji pia kama serikali haioni umuhimu wa kumaliza mgogoro huo kwa wakati ili kurejesha haki ya wafanyakazi hao.
Lutevele amerejea kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kuacha tabasamu kwa Watanzania, akisisitiza kuwa wafanyakazi hao wanastahili kulipwa fidia yao haraka baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amesema madai hayo yanatokana na mchakato wa ubinafsishaji wa kiwanda hicho mwaka 2004 uliosababisha baadhi ya wafanyakazi kupunguzwa kazi.
Ameeleza kuwa mwekezaji tayari amelipa sehemu ya madai yanayomhusu, huku serikali ikibeba jukumu la upande wake kama mmiliki wa awali kabla ya ubinafsishaji.
Londo ameongeza kuwa serikali ilitenga fedha kwa ajili ya madai hayo mwaka wa fedha 2017/2018, lakini baadhi ya wadai walikataa kupokea wakidai kiwango kilichotolewa hakikutosheleza.
Hata hivyo, amesema serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kumaliza mgogoro huo, huku akibainisha kuwa suala hilo bado liko katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi.

You Might Also Like

Makala: Hakuna Kupita Bila Kupingwa

CHAUMMA Kuunda Mamlaka ya Mazao ya Kimkakati – Salum Mwalim

Uwekezaji wa TIB Wachangia Kuongezeka kwa Ajira

Ajali Yakatisha Maisha Ya Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji TANESCO, Dereva Wake 

Elimu Itolewe Kuhusu Ufahamu Wa Kuwepo Kwa Fedha Maalum – Ridhiwani

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kasekenya: Barabara ya Kakonko–Muhanga Ipo Katika Hatua za Awali za Kujengwa
Next Article Wananchi wa Kasulu Vijijini Wananufaika na Uwekezaji Makere Forest Reserve
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ubunifu Wa Majengo Watakiwa Kuzingatia Tija Na Gharama Nafuu
Habari April 11, 2026
Waziri Ulega aridhishwa na miradi ya dharura TANROADS
Habari April 11, 2026
Mbunge Majule ataka wanawake wapewe elimu ya fedha na mitaji
Habari April 11, 2026
Mbunge Msita Ataka Ukarabati Wa Haraka Barabara Zilizoharibiwa Na Mvua
Habari April 11, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?