MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mavunde: Makaa ya Mawe Ni Injini ya Maendeleo ya Viwanda
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mavunde: Makaa ya Mawe Ni Injini ya Maendeleo ya Viwanda
Habari

Mavunde: Makaa ya Mawe Ni Injini ya Maendeleo ya Viwanda

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, amesema kuwa makaa ya mawe yana nafasi ya kimkakati katika kuharakisha mageuzi ya uchumi wa Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda.
Ameeleza kuwa rasilimali hiyo si tu chanzo cha nishati, bali pia ni mhimili muhimu katika kuongeza thamani ya madini na malighafi nyingine za viwandani.
Akizungumza Machi 30, 2026 katika kikao na wadau wa makaa ya mawe kilichofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Madini jijini Dodoma, Mavunde amesisitiza kuwa matumizi sahihi ya makaa ya mawe yanaweza kusaidia kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje,
Kuongeza uzalishaji wa ndani na kuimarisha mnyororo wa thamani katika sekta mbalimbali, zikiwemo nishati, viwanda na madini.
Habari Picha 11638
Amebainisha kuwa Serikali itaendelea kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wadau wa sekta hiyo ili kuhakikisha inakua kwa kasi na ufanisi zaidi.
“Makaa ya mawe ni mhimili muhimu katika maendeleo ya viwanda. Tunahitaji kuongeza uzalishaji na kuhakikisha matumizi yake yanaongeza thamani ndani ya nchi,” amesema Mavunde.
Habari Picha 11639
Katika kikao hicho, Waziri amepokea changamoto mbalimbali kutoka kwa wachimbaji na wafanyabiashara, zikiwemo gharama za uzalishaji, usafirishaji na upatikanaji wa masoko.
Ameahidi kuwa Serikali itazifanyia kazi changamoto hizo kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.
Aidha, amesisitiza kuwa upangaji wa bei elekezi utafanyika kwa ushirikishwaji wa wadau wote ili kulinda maslahi ya sekta.
Habari Picha 11637
Wadau wa makaa ya mawe waliipongeza Serikali kwa kuwashirikisha katika majadiliano, wakieleza kuwa hatua hiyo imeongeza uwazi na imani katika uendeshaji wa sekta.
Wameahidi kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya ndani na kuongeza mapato ya Taifa.
Kwa upande mwingine, Mavunde amewahimiza wadau kuanzisha chama kitakachowaunganisha ili kurahisisha uratibu wa shughuli zao na kushughulikia changamoto kwa pamoja.
Habari Picha 11640
Katika kuimarisha viwanda vya ndani, amesema Kampuni ya A1 Steels Tanzania Ltd inapanga kujenga kiwanda cha chuma Dodoma, kitakachotumia takribani tani 20,000 za makaa ya mawe kwa mwaka.
Mradi huo unatarajiwa kuchochea ajira, kuongeza thamani ya madini na kuimarisha uchumi wa Taifa.

You Might Also Like

Samia Kukagua Barabara Ya Mzunguko, Uwanja Wa Ndege Msalato Kesho

Kamati Ya Bunge Ustawi Na Maendeleo Ya Jamii Yaridhishwa Wananchi Wanavyofikiwa

Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima

Serikali Yawekeza Katika Utafiti wa Alizeti, Wakulima Wapate Mbegu Bora

Ulega Ataka Ushirikiano Miradi Ya Kimkakati Ikamilike Kwa Wakati

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Programu Mpya ya TPHPA Yalenga Usalama wa Mazao Sokoni
Next Article Mafunzo ya Usalama wa Mabwawa Kuimarisha Ulinzi wa Mazingira
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Kijaji: Huduma ya Kudungwa na Nyuki Kuongeza Kinga Yavutia Bungeni
Habari May 15, 2026
Serikali  Kutumia Fursa  ya AFCON,  Miss World Na IPU Kukuza Utalii Nchini
Habari May 15, 2026
TFS Yavunja Rekodi Utalii Wa Misitu,Mapato Yapaa Kwa Asilimia 43
Habari May 15, 2026
Serikali Kuimarisha Uvuvi Bahari Kuu Kupitia TAFICO
Habari May 14, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?