MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mafunzo ya Usalama wa Mabwawa Kuimarisha Ulinzi wa Mazingira
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mafunzo ya Usalama wa Mabwawa Kuimarisha Ulinzi wa Mazingira
Habari

Mafunzo ya Usalama wa Mabwawa Kuimarisha Ulinzi wa Mazingira

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WIZARA ya Maji kwa kushirikiana na taasisi binafsi imeandaa mafunzo ya usalama wa mabwawa yatakayolenga kuhakikisha miundombinu hiyo inaendelea kuwa salama kwa matumizi yaliyokusudiwa hapa nchini.
Akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Maji, Mtumba jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Robert Sunday, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, alisema mafunzo hayo yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Oktoba 21 hadi 23, 2026.
Alitaja taasisi zinazoshirikiana na Wizara hiyo kuwa ni Chemba ya Migodi Tanzania (CMT) pamoja na Kampuni ya Uhandisi ya City, akibainisha kuwa ushirikiano huo unalenga kuimarisha uelewa wa kitaalamu kuhusu usalama wa mabwawa.
Sunday ameeleza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wadau na wataalamu wa mabwawa ili kuhakikisha usanifu, ujenzi na uendelezaji wa mabwawa ya maji pamoja na mabwawa ya tope sumu unazingatia viwango vinavyotakiwa.
 Amesisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda mazingira na vyanzo vya maji.
Washiriki wanaotarajiwa kushiriki ni kutoka serikalini na sekta binafsi, wakiwemo wamiliki wa mabwawa makubwa, wataalamu waliosajiliwa wa mabwawa pamoja na wale wanaohusika na usimamizi wa mabwawa ya maji na tope sumu.
Mafunzo hayo yataongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Usalama wa miundombinu ya mabwawa kuanzia hatua ya usanifu, utumiaji hadi ufungaji.’
Aidha, ametumia fursa hiyo kuwaalika watunga sera, wataalamu, taasisi mbalimbali na watu binafsi wanaojishughulisha na mabwawa kujisajili kushiriki mafunzo hayo ili kuongeza ufanisi na usalama wa miundombinu hiyo muhimu.

You Might Also Like

Masauni Akabidhi Polisi Magari 77

Simbachawene: Simu za mkononi zinaondoa umakini kwa watumishi wa umma

Washauriwa Kutumia Mbegu Zinazokabiliana Na Mabadiliko Ya Tabia Nchi

Mramba Afungua Mafunzo Ya Teknolojia Ya Nishati Jua Kwa Watalaam

Kamati Ya Bunge  Yaridhishwa Na Ujenzi Wa Jengo La Kituo Cha Zimamoto, Mtumba

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mavunde: Makaa ya Mawe Ni Injini ya Maendeleo ya Viwanda
Next Article Serikali Yaendelea Kuimarisha Sekta Ya Utalii, Mapato Yaongezeka
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

VETA kumpa nafasi Igobeko kuongeza ujuzi na kuwawezesha wengine
Habari August 23, 2026
Airtel Yajenga Darasa La Fursa Katika Shule Ya Sekondari Magaoni,Tanga
Habari August 23, 2026
Bunifu ya dawa ya mayai yapunguza hasara kwa wafugaji wa kuku
Makala August 22, 2026
Dkt Yonaz Awakumbusha Vijana Kulinda Afya Zao Katika Mapambano Dhidi Ya Ukimwi
Habari August 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?