Na Mwandishi Wetu
KIGOMA: IKIWA zimebakia siku mbili kabla ya kufungwa kwa uandikishwaji katika Daftari la Mkazi Oktoba 20, 2024 wananchi wametakiwa kutumia muda ulobaki kujiandikisha.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Dkt. Semistatus Mashimba amewataka wananchi hao kujiandikisha ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024.
Amesema hayo alipokuwa akizungumza katika Kituo Kimoja cha Radio, mkoani Kigoma.
Amesema licha ya msimu huu kuwa wa kilimo mkoani hapo,mchakato wa uandikishaji unaendelea vizuri.
“Mwanzoni uandikishwaji ulikuwa na changamoto kwa sababu baadhi ya wananchi walijikita kwenye maandaizi ya kilimo ili kuandaa mashamba yao,
Lakini hivi sasa uandikishwaji unaaendelea vizuri kwa wananchi kwenda kujiandikisha katika vituo mbalimbali tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzoni.
Pia amesema idadi ya kujiandikisha kwa vijana ilikuwa si ya kuridhisha lakini kupitia hamasa mbalimbali zilizofanywa kwa sasa idadi yao inaridhisha tofauti na awali.