MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading:
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari >
Habari

Author
By Author
Share
2 Min Read

VETA Dodoma Yatengeneza Biskuti Za Uwele, Yahamasisha Vijana Kujiunga Kupata Mafunzo

Na Lucy Lyatuu,Dodoma

MAMLAKA Ya Elimu Na Mafunzo Ya Ufundi Stadi (VETA), Dodoma inahimiza wananchi hususani vijana kujiunga na Mamlaka hiyo ili kujifunza namna ya kutumia mazao yanayopatikana kwenye maeneo wanauoishi na kutengeneza bidhaa tofautitofauti zenye kuwapatia kipato.

Mwalimu wa Chuo cha VETA Dodoma,Amina Juma amesema hayo wakati akizungumza katika maoneshonya Nanenane jijini humo na kuongeza kuwa Mamlaka hiyo imeweza kutumia uwele kutengeneza biskuti na keki ambazo kiafya zina manufaa.

Kuhusu manufaa kwa bidhaa za uwele amesema wametumia zao hilo kutengeneza bidhaa hizo kuonesha jinsi lilivyo na faida kwenye mwili wa binadamu kwa kuimarisha mifupa na hata viungo kwa ujumla.

” Uwele unaimarisha afya ya mwili kwa watoto na wazee na hata kupunguza homa za mifupa,” amesema Amina na kuwataka wananchi kufika katika banda la VETA ili kupata elimu na manufaa ya zao hilo ambalo hupatikanankwa wingi mkoani humo.

Amesema pia uwele husaidia kuimarisha afya ya moyo kwa kuwa ndani yake kuna madini ya potasium na magneziam kwa wingi ambapo huwasaidia kupata ahueni na pia kusaidia wenye kisukari pia kupata nafuu kuyokana na chakula kuchakatwa vyema mwilini.

Amina ameongeza kuwa uwele ni zao linalopatikana kwa wingi na wameamua kulitumia kutengeneza bidhaa hizo ambazo pia zina manufaa kwa mwili wa binadamu.

Mbali na zao hilo,Amina amesema chini ya kitengo cha uhudumu wa chakula na vinywaji ndani ya Idara ya Hotel Menejimenti katika Mamlaka hiyo hufundisha vijana namna ya kujiajiri katika kitengo hicho.

Amesema wamekuwa wakifundisha vijana kujiandaa na soko la hotel wakitoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu wakifundisha namna ya kutumia mazao yanayoweza kutengeneza bidhaa mbalimbali,kuongezea thamani ya mazao na kuwataka vijana kujiunga na mafunzo hayo.

You Might Also Like

Ushiriki Wa Wanawake, Wasichana Katika Sayansi Ni Mdogo

MSD, SALAMA Zaunganisha Nguvu Kuboresha Sekta ya Afya SADC

Wakazi Wa Ntyuka Wataka Kiongozi Mchapakazi

VETA Dodoma Waleta Mashine Kurahisishia Upekechuaji Wa Alzeti

Serikali Kuwasilisha Bungeni Nyenzo Kuu Tatu Zitakazowezesha Utekelezaji Dira 2050

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TAMCU Yapaa Kwa Uwekezaji,Yafikisha Thamani Ya Sh  Bilioni Tano
Next Article Nishati Ni Chachu Ya Kilimo, Uchumi Na Maendeleo  Ya Vijijini – Saidy
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Nishati Ni Chachu Ya Kilimo, Uchumi Na Maendeleo  Ya Vijijini – Saidy
Habari August 3, 2026
TAMCU Yapaa Kwa Uwekezaji,Yafikisha Thamani Ya Sh  Bilioni Tano
Habari August 3, 2026
Bidhaa Zinazozalishwa Nchini Zifikie Viwango Vinavyotakiwa Kukidhi Masoko-Balozi Mussa
Habari August 2, 2026
 DIB Kulinda Fedha Za Wawekaji Amana Katika Taasisi Za Fedha
Habari August 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?