Na Mwandishi Wetu
ILEJE: MBUNGE wa Ileje ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya, ametoa pole kwa wananchi walioathiriwa na moto ulioteketeza mashamba ya miti wilayani humo, huku akitoa msaada wa fedha za matibabu kwa baadhi ya waathirika.
Kasekenya amewataka wananchi kuendelea kushirikiana kuwapatia waathirika hao hifadhi na huduma za matibabu wakati Serikali ikiendelea na juhudi za kutafuta misaada zaidi kwa ajili yao.
Akiwa katika ziara ya jimboni humo, mbunge huyo amekabidhi misaada mbalimbali, ikiwemo fedha za kugharamia matibabu kwa baadhi ya waathirika, huku akisisitiza umuhimu wa jamii kusaidiana wakati wa majanga.

Moto huo, unaodaiwa kuzuka Oktoba 23, 2026, umeteketeza mashamba ya miti ya wananchi katika vijiji vya Chilemba, Lali, Shikunga na Ibaba.
Kutokana na athari hizo, wananchi walioathirika wameiomba Serikali kuwapatia miche ya miti ili waweze kuanzisha upya mashamba yao mara mvua zitakapoanza.





Maoni 0
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!