Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 5

Kija: Samia Aonesha Uongozi Wa Vitendo Mwaka Mmoja

Na Lucy Ngowi

DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Katoro mkoani Geita, Kija Ntemi (CCM), amesema mwaka mmoja wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika awamu ya pili ya uongozi umeambatana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, akitaja hatua hizo kuwa ushahidi wa uongozi unaozingatia vitendo.

Amesema katika kipindi hicho Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya kimkakati inayolenga kuboresha maisha ya wananchi, kuimarisha uchumi na kuongeza fursa za kiuchumi katika sekta mbalimbali.

Akizungumza kuhusu mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia tangu alipoapishwa Novemba 3, 2025, Kija ametaja kukamilika kwa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere na Daraja la Magufuli kuwa miongoni mwa hatua muhimu zilizopatikana.

Habari Picha 14258

Amesema kukamilika kwa Daraja la Magufuli kumeimarisha mawasiliano kati ya mikoa ya Mwanza na Geita kwa kurahisisha safari na kupunguza muda wa kuvuka Ziwa Victoria.

Aidha, amesema Serikali imeendelea kuimarisha sekta ya madini kwa kuweka mazingira yanayowawezesha wachimbaji wadogo kufanya shughuli zao katika maeneo mbalimbali nchini, hali inayochochea ushiriki wa wawekezaji na wafanyabiashara wengine katika sekta hiyo.

Ametaja pia kuendelea kwa ujenzi wa Daraja la Magu–Musoma, akisema mradi huo utakapokamilika utaongeza fursa za usafiri na kuimarisha mawasiliano katika maeneo husika.

Kija ameongeza kuwa uzinduzi wa Jiji la Serikali Mtumba jijini Dodoma ni hatua nyingine katika utekelezaji wa mkakati wa kuhamishia shughuli za Serikali makao makuu ya nchi.

“Dkt. Samia ni Rais ambaye anaonesha kwa vitendo kile anachotaka kufanya kupitia utekelezaji wa miradi na mahitaji ya wananchi,” amesema.

Amesema anaunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kumtakia Rais Samia afya njema katika kuendelea kulitumikia taifa.

Pia amewahimiza wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo na kutumia fursa zinazotokana na miradi inayotekelezwa nchini.

Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.