Na Lucy Lyatuu
SHIRIKA la Maendeleo ya Wafanyakazi (WDC) linatarajiwa kuzindua mradi wa jengo lake la uwekezaji lililoko jijini Arusha Novemba mwaka huu.
Tayari maboresho ya jengo hilo lenye gorofa nne yanakaribia kukamilika ifikapo Octoba 2024 yakitarajiwa kugharimu sh bilioni 2.5.
Meneja Mkuu wa WDC,Muchunguzi Kabonaki amesema hayo wakati akizungumza na gazeti la MFANYAKAZI kuhusu maendeleo ya uboreshaji wa mradi huo.

Amesema kwa jiji la Arusha yapo majengo pacha yanayokarabatiwa kwa gharama ya sh bilioni 2.5 Hadi kukamilika kwake ambao ni mradi wa kuongeza Mapato na kuongeza Fursa za biashara.
Kabonaki amesema ukarabati wa mradi wa Arusha ulianza June 2023 na unatarajiwa kukamilika Oktoba 2024 na kuzinduliwa rasmi.
Amesema lengo la mradi ni kuzalisha zaidi ya bilioni 1.5 kwa mwaka kwani una mita za mraba zaidi ya 5000 ambazo zitapangishwa na zizalishe mil 80 kwa mwezi.
Amesema jengo hilo la gorofa nne lina vyumba vikubwa vya kupangisha kwa ajili ya biashara lakini pia hotel yenye vyumba vya kulala,ukumbi pamoja na mgahawa.
Kabonaki amesema mbali na mradi huo pia WDC iinatarajiwa kuwa nanuwekezaji mkubwa katika mhi wa Dodoma utakaogharimu sh bilioni 50.
Amesema mradi huo unatarajiwa kuanzia Januari 2025 ikiwa ni kujenga ghorofa za kuishi na usanifu unatarajiwa kuqnza Januari.