Na Lucy Lyatuu,Tanga
SHIRIKA la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limewatambua na kuwapongeza wanawake vinara wa kilimo nchini Tanzania kupitia utoaji wa tuzo maalum zilizofanyika jijini Tanga katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani.
Hatua hiyo imelenga kuenzi mchango mkubwa wa mwanamke mkulima katika uzalishaji wa chakula, biashara ya kilimo, na uboreshaji wa lishe katika ngazi ya kaya.
Akizungumza katika hafla ya kuwatambua katika viwanja vya Usagara, Mwakilishi Mkazi wa FAO,Charles Tulahi amesema FAO inatambua mchango wa mwanamke mkulima katika kuhakikisha uwepo wa chakula katika familia.

Amesema FAO inathamini jitihada za mwanamke mkulima kwa kuzingatia mifumo yote ya upatikanaji wa chakula bora na kwamba wadau wa chakula wanakaribishwa kuwekeza kaa wanawake wakulima kuhakikisha kuinua kiwango cha chakula na lishe.
Amesema kufikia dira ya taifa ya maendeleo 2050 wanawake wanatakiwa kuwa nfuzo muhimunkwa chakula na lishe,kuwa na uzalishaji bora,lishe bora na mazingira bora.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Pangani Mwanaidi Rajabu amesema bado wanawake wengi wanakabiliwa na chagamoto mbalimbli iiiwemo ukosefu wa teknolojia za kisasa ambayo itasaidia kupata elimu ya kuboresha maisha yao.
Amewataka wadau wa kilimo kuwekeza kwa wanawake wakulima kuelimishwa kuhusu miongozo ya usalama wa chakula na lishe na kuimarisha umuhimu wa fursa sawa kwa wanawaake.
“Wanawake wawezeshwe kuhusubteknolojia kwa kuwa inaweza kuongeza kipato,kukuza ubunifu wao ,”amesema na kuongeza pia wanawake washiriki karika maamuzi yanayohusu kilimo.

Hata hivyo amesisitiza fursa za wanawake kutumika kwao pekenyao kwa kuwa wao ndio wanaojua wanaweka akjba kiasi gani ya chakula, na hata mahitaji ya kesho ya familia.
Naye Mratibu wa dawati la jinsia la FAO,Jane Msagati amesema katika ngazi ya kimataifa, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeitumia FAO kuongoza maadhimisho ya Mwaka wa Kimataifa wa Mwanamke Mkulima (IYWF 2026) ili kuongeza uwekezaji na kuondoa mapengo ya kijinsia kwenye sekta hiyo.

Amevitaja Vigezo Vilivyotumika Kuwatambua wanawake wakulima vinara kuwa ni pamoja na Matumizi ya mbolea za asili, Wanawake wanaotumia mbinu salama kupunguza athari za kemikali kwenye udongo na chakula.
Amesema kigezo kingine ni Uzalishaji wa mboga mboga, Uhodari katika kilimo cha mazao mbalimbali ya mboga mboga kwa ajili ya chakula na biashara na Ufugaji na mnyororo wa thamani: Ushiriki mzuri katika ufugaji wa kuku, ng’ombe wa maziwa, na mbuzi unaosaidia kuongeza lishe na kipato cha familia.

Maoni 0
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!