MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Elimu Ya Nishati Safi Ya Kupikia Yawafikia Maofisa Dawati Ngazi Ya Mikoa Na Halmashauri
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Elimu Ya Nishati Safi Ya Kupikia Yawafikia Maofisa Dawati Ngazi Ya Mikoa Na Halmashauri
Habari

Elimu Ya Nishati Safi Ya Kupikia Yawafikia Maofisa Dawati Ngazi Ya Mikoa Na Halmashauri

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

WIZARA  ya Nishati imeanza kutoa elimu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia  kwa  Maofisa Dawati wa Nishati Safi ya Kupikia ngazi ya mikoa na halmashauri  kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia pamoja na  kuwawezesha Maafisa Dawati kutambua majukumu yao katika utekelezaji wa mkakati..

Akifungua  mafunzo hayo, wilayani Kibaha mkoani Pwani,  Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa  Pwani,  Hadija Mruma ameipongeza Wizara ya Nishati kwa jitihada mbalimbali inazochukua kwa vitendo katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini mojawapo ikiwa ni kuhakikisha elimu na vifaa vya nishati safi ya kupikia vinafika hadi ngazi za Mikoa, Halmashauri na Vijiji.

Ameeleza kuwa Mkoa wa Pwani unachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachi wanatumia nishati safi ya kupikia katika ngazi ya taasisi, kaya n.k akitoa mfano kuwa asilimia 76 ya taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 mkoani humo zimeshahamia kwenye nishati safi ya kupikia.

Habari Picha 10202

 

Aidha, amewapongeza Watendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini ( REA)  ambao wanashirikiana na Mkoa wa Pwani kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo utoaji mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati,  Ngereja Mgejwa ameeleza kuwa mafunzo kuhusu Nishati Safi ya Kupikia yameanza kutolewa wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa kuhusisha Mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Tanga.

Ameongeza kuwa, elimu ya nishati safi ya kupikia itaendelea kutolewa kwa Maofisa Dawati wa Nishati Safi ya Kupikia katika mikoa mingine iliyosalia kwani lengo ni kutoa elimu husika katika  Mikoa yote 26 pamoja na Halmashauri zake.

Amesema kuwa suala la matumizi ya nishati safi ya kupikia ni kipaumbele cha nchi na dunia kwa ujumla ili kuondokana na athari zake katika  mazingira, afya na kiuchumi.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Wizara ya Nishati,  Neema Mbuja ameeleza kuwa mafunzo yanayotolewa kwa maafisa dawati hao yanahusisha pia masuala ya Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya Kupikia.

Habari Picha 10203

 

Ameeleza kuwa ili kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu nishati safi ya kupikia ni muhimu maafisa dawati hao wakafahamu njia za mawasiliano zitakazowasadia kufikisha elimu  na  jumbe zitakazotumika kuendana na maeneo wanayoyasimamia.

Ameongeza kuwa uwepo wa Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya Kupikia unatoa mwongozo wa namna wadau watakavyoshirikiana kutoa elimu kwa umma ili kuondoa dhana potoshajii (misconception) kuhusu nishati safi ya kupikia na kubadili mitazamo hasi kuwa chanya kwa lengo la kuleta mabadiliko katika utekelezaji wa ajenda ya kitaifa ya nishati safi ya kupikia.

 

You Might Also Like

Nchemba Afungua Mafunzo Ya PAC

Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija

Serikali Kupeleka Umeme Maeneo Ya Kimkakati

Kafulila: Deni La Taifa Ni Himilivu

Makamanda Wa Polisi Msiende Nyumbani na Vyeo Vya Ukamanda

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wananchi wahamasishwa kuandika historia mpya kupitia kura
Next Article Twendeni Tukapige Kura Ya Ukombozi, CHAUMMA Yahitimisha Kampeni
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Twendeni Tukapige Kura Ya Ukombozi, CHAUMMA Yahitimisha Kampeni
Habari October 28, 2025
Wananchi wahamasishwa kuandika historia mpya kupitia kura
Habari October 25, 2025
Shibuda: WanaMaswa jitokezeni kupiga kura bila woga
Habari October 25, 2025
Daktari: Saratani ya Matiti Inazuilika, Inatibika
Habari October 25, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?