MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Miradi 10 Ya Kimkakati TPA Kuinua Uchumi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Miradi 10 Ya Kimkakati TPA Kuinua Uchumi
Habari

Miradi 10 Ya Kimkakati TPA Kuinua Uchumi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read

Na Danson Kaijage

DODOMA: SERIKALI kupitia bandari inatekeleza mapendekezo ya mpango kabambe ya maendeleo ya bandari nchini (2020 – 2045) na programu ya uboreshaji na uendeshaji wa bandari ambao ni mpango wa kitaifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Plasduce Mbossa amesema hayo alipozungumza na Waandishi wa Habari.

Amesema katika Programu hiyo bandari imejipanga  kutekeleza miradi 10 ya kimkakati itakayoleta tija kwa taifa na kwa ustawi wa Bandari.

Miongoni mwa miradi hiyo ameitaja kuwa ni Mradi wa kupokelea na kuhifadhia mafuta, ambapo unagharimu dola za kimarekani million 265, na utekelezaji wake umefikia asilimia 17.

Amesema mradi huo ukikamilika utapunguza siku za kuhudumia meli zenye ujazo wa 150,000 DWT kutoka siku 10 mpaka tatu.

Mradi mwingine utagharimu dola za kimarekani milioni 119.9 ambao ni ujenzi wa kituo cha reli na mtandao wake ndani ya bandari ya Dar es Salaam.

“Mradi huu ukikamilika utapunguza kiwango cha asilimia 98 cha shehena inayotoka bandarini kwa kutumia njia ya barabara na kupelekea kutatua tatizo la msongamano wa malori ndani na nje ya bandari,” amesema.

Pia ameongeza kwamba, ujenzi wa gati mbili zenye jumla ya urefu wa mita 500, utagharimu dola za kimarekani million 250, kwamba ukikamilika utawezesha ufungaji wa meli mbili zenye ukubwa wa 50,000 DWT katika gati hizo kwa wakati mmoja.

Vile vile amesema mradi wa ujenzi wa bandari maalum ya kisiwa – mgao mkoani Mtwara kwa ajili ya kuhudumia shehena chafu, utagharimu dola za kimarekani milioni 171.

Maelezo yake ni kwamba, mradi huo umelenga kuepusha athari za kimazingira na kuondoa changamoto zinazotokana na kuhudumia mizigo katika bandari ya Mtwara.

Pia amesema uboreshaji wa gati namba nane hadi 11 yenye jumla za mita 720 pamoja na maeneo ya kuhifadhia makasha, utagharimu dola za kimarekani million 220.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa miradi mingine ni  uendelezaji wa bandari kavu eneo la Kurasini na Ihumwa – Dodoma, itagharimu dola za kimarekani milioni 157.

Amesema mradi wa uendelezaji bandari ya Kigoma unagharimu dola za kimarekani milioni 48.82, unalenga kuimarisha uchumi wa ushoroba wa kati.

Vile vile ujenzi wa gati maalum la kuhudumia makasha na Gati la mafuta – Bandari ya Tanga utakaoghrimu dola za kimarekani milion 201.

“Ujenzi wa gati namba 12 hadi 15 utakao gharimu dola za kimarekani milion 591.564 unaolenga kuongeza ufanisi wa bandari ya DSM.

“Ujenzi wa bandari mpya ya Mbegani Bagamoyo utakao gharimu dola za kimarekani bilion 1.5.”amesema.

 

 

You Might Also Like

Tanzania Ipo Tayari Soko la Pamoja kuuziana Umeme – Biteko

Rais Samia akunwa na Tarura

Miradi ya Maendeleo Isimamiwe kwa Uadilifu

DIT Mwanza   Kutoa Kozi Ya Kuchakata Ngozi

TARI Yatikisa Sabasaba Na Mti Wa ‘Allspice’

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TRC, Wananchi Burundi Wakutana Utekelezaji Mradi wa SGR
Next Article Ridhiwani Kikwete Azindua Miradi Ya Thamani Ya Bil. 1.7 Songwe
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Habari July 30, 2026
Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Habari July 30, 2026
Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa Msongo Wa Kilovolti 400 Chalinze -Dodoma Mbioni Kukamilika
Habari July 29, 2026
Kutoka Wazo Rahisi Hadi Mapinduzi ya Kilimo: Safari ya Rafiki Planter Inayosimulia Miaka 40 ya COSTECH
Makala July 28, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?