Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 12

ASA Yaleta Mbegu Za Mahindi,Mpunga Zenye Kustahimili Mvua Nyingi Na Ukame

Na Lucy Lyatuu,Tanga

WAKALA wa Mbegu Za Kilimo Tanzania (ASA) Umeleta mbegu za mpunga na mahindi aina ya T105 ambayo inaweza kukabiliana na  changamoto ya mvua nyingi hata ukame.
Hayo yamesemwa na Suzan Ludovick kutoka ASA wakati akizungumza katika kilele cha siku ya chakula duniani ambayo maadhimisho yake yamefanyikia jijini humo katika viwanja vya Usagara.
Amesema ASA ambayo pia inazalisha   na kusambaza mbegu ina mbegu za aina mbalimbali ikiwemo za nafaka,mbogamboga na mikunde pamona na  miche ya matunda.
Habari Picha 14159
Amesema mbegu ya mpunga waliyonayo inafanya vizuri kwenye mabonde ambayo haijitaji maji mengi na kuwashauri wakulima kutumia mbegu bora ambazo zimeboreshwa.
Amesema mbegu hizo zinastahimili magonjwa, mvua nyingi na ukame na kwamba tayari zinapatikana maeneo yote kupitia mawakala wa ASA nchi nzima.
“ASA inawajibu wa kuhakikisha mkulima anapata mbegu bora kwa bei nafuu nankwa wakati,” amesema Suzan.
Kwa upande wake Ofisa Kilimo wa ASA, Emanuel Nyampwani amesema amewataka wakulima kutumia mbegu hizo za mpunga aina ya Saro 5 na mbegu ya mahindi T105 ili kwa kuwa zinavumilia mvua njingi na magonjwa.
Amewataka wakulima kutumia mbegu hizo kwa kuwa zinatoa mavuno mengi.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.