MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: ARU  Wabuni Utengenezaji Vigae Kutumia  Chupa Za Plastiki Za Vinywaji Vya Kuongeza Nguvu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > ARU  Wabuni Utengenezaji Vigae Kutumia  Chupa Za Plastiki Za Vinywaji Vya Kuongeza Nguvu
Habari

ARU  Wabuni Utengenezaji Vigae Kutumia  Chupa Za Plastiki Za Vinywaji Vya Kuongeza Nguvu

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Tanga
MWANAFUNZI wa Chuo  Kikuu Cha Ardhi (ARU) Vinod Valence amebuni utengenezaji wa vigae vinavyotokana na chupa za plastiki za rangi baada ya kuzirejelesha.
Chupa zinazotumika ni za rangi zinazotumika kuweka vinywaji vya kuongeza nguvu,ambazo soko lake la urejelezaji  ni dogo hiku zikiachwa kuchafua mazingira.
Valence  amesema hayo wakati akizungumza katika banda la Ardhi katika maadhimisho ya wiki ya Elimu Ujuzi Na Ubunifu 2026 yanayofanyika  katika viwanja vya Usagara Tanga.
Kuhusu mchakato wa utengenezaji, chupa za plastiki za rangi huyeyushwa na kupata mchanganyiko unaochanganywa na mchanga wa kawaida.
“Mchanganyiko huo huwekwa kwenye mold mbalimbali kulingana na ukubwa na mahitaji ya mteja, na hatimaye kutengeneza vigae vya ukubwa tofauti,” amesema.
Amesema  vigae hivyo vimetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kuwekwa kwenye kuta za vyoo, mabafu na jikoni, na si kwa matumizi ya sakafuni kutokana na sehemu yake ya juu kuwa laini.
Ameongeza kuwa, ubunifu huo unalenga pia kutoa bidhaa yenye bei nafuu ambayo inaweza kumudu kutumiwa na wananchi wenye viwango tofauti vya kipato.
Aidha amesema mbali na kutatua changamoto ya taka za plastiki, ubunifu huo unaweza kutoa soko kwa wakusanyaji wa chupa za plastiki, ambao wataweza kukusanya chupa hizo na kuzipeleka kwa ajili ya kuchakatwa na kuzalisha bidhaa mpya.
Kuhusu hatua ya kupata ithibati, Valence amesema kwa sasa wanaendelea na uzalishaji wa vigae hivyo kwa wingi ili kufanya majaribio zaidi, kabla ya kuwasilisha bidhaa hiyo kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kuthibitishwa kwa matumizi ya sokoni.
“Tayari tumefanya majaribio ya awali kwa kutumia vigae hivyo kwenye kuta za vyoo, mabafu na jikoni, na tumepata maoni kutoka kwa wananchi katika maonyesho mbalimbali tunayoshiriki,” amesema.

You Might Also Like

TEA, UNICEF na Canada waendeleza mageuzi ya elimu Sikonge

Umeme Jua Kuchoche Uchumi Maeneo Ya Vijijini

Serikali Imetoa Ruzuku Ya Asilimia 20 Hadi 50 Kwenye Mitungi YA Gesi – Kapinga

Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo 2030

Bajeti Yadhihirisha Uhakika Wa Nishati Nchini

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kutoka Sh. Milioni 20 Hadi Uchumi Wa Bilioni : Ubunifu Wa Dkt. Cecilia China Unaunganisha Korosho, Mifugo, Viwanda Na Ajira
Next Article BRELA Yatoa Elimu ya Hataza na Alama za Biashara kwa Wabunifu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

BRELA Yatoa Elimu ya Hataza na Alama za Biashara kwa Wabunifu
Habari August 21, 2026
Kutoka Sh. Milioni 20 Hadi Uchumi Wa Bilioni : Ubunifu Wa Dkt. Cecilia China Unaunganisha Korosho, Mifugo, Viwanda Na Ajira
Makala August 21, 2026
Tanzania Yanoa Vijana Kuwa Mabingwa Wa Ujuzi Afrika,Duniani Kupitia WorldSkills
Habari August 20, 2026
NeST Yaongeza Uwazi Na Ufanisi Katika Ununuzi Wa Umma
Habari August 20, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?