Na Lucy Ngowi
AJALI ya gari iliyotokea Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, imekatisha maisha ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Gissima Nyamo – Hanga, na dereva wake Muhajiri Mohamed Haule.
Ajali hiyo imetokea leo Aprili 13, 2025.
Kurugenzi ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja TANESCO, imetoa taarifa hiyo na kusema, taarifa zaidi zitatolewa.