MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Polisi Dar Wakamata Magari 15  Yasiyo na Usajili Rasmi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Polisi Dar Wakamata Magari 15  Yasiyo na Usajili Rasmi
Habari

Polisi Dar Wakamata Magari 15  Yasiyo na Usajili Rasmi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeendesha msako maalum kuanzia Agosti 18 hadi 25, mwaka huu 2025, na kukamata magari 15 yaliyokuwa yakiendeshwa bila namba rasmi za usajili.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari.
Habari Picha 9245
“Magari haya yalikuwa na namba bandia za usajili aina ya SSH 2530, kinyume na Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 ya mwaka 1973 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2023.
“Kuendesha chombo cha moto bila usajili rasmi ni kosa kubwa linalohatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara,” amesema Kamanda Muliro.
Katika hatua nyingine ya kuhakikisha usalama wa raia na kupambana na biashara haramu, Kamanda Muliro amesema mnamo Agosti 11, 2025, alikamatwa Ramadhani Makala, mkazi wa Tabata, kwa tuhuma za kusafirisha magunia ya mchele yaliyochanganywa na mizigo ya bangi.
Habari Picha 9246
“Tulimkamata mtuhumiwa akiwa anatumia gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T.733 AGT kusafirisha magunia 13 ya bangi yenye uzito wa takribani kilo 239 kutoka Morogoro kuelekea Dar es Salaam.
“Mizigo hiyo ilikuwa imefichwa kati ya magunia ya mchele kwa lengo la kudanganya vyombo vya usalama,” amesema Kamanda Muliro.
Aidha, kati ya Agosti 12 hadi 20, 2025, Jeshi la Polisi pia liliwakamata watuhumiwa wawili waliokuwa wakijihusisha na wizi wa mali mbalimbali za pikipiki. Watuhumiwa hao ni Hassan Hamis, mkazi wa Candle, na Elia Mapunda, mkazi wa Goba Njia Nne.
“Watuhumiwa walikamatwa wakiwa na vipuli vya pikipiki pamoja na pikipiki sita, mali zinazodhaniwa kuwa za wizi. Upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao mzima unaohusika na wizi wa pikipiki jijini Dar es Salaam,” amesema.
Kamanda Muliro amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na jitihada za kuhakikisha amani na usalama vinadumishwa, huku akitoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa za uhalifu au viashiria vyake mapema.
Jeshi la Polisi limeeleza dhamira yake ya kuendeleza misako na doria za mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya jiji ili kudhibiti uhalifu, na kuhakikisha sheria inafuatwa kikamilifu na kila mwananchi kwa ustawi wa taifa.

You Might Also Like

Silinde Akabidhi Nyaraka za Kufungua Masoko Mapya Nje ya Nchi

Dada wa kazi aliyejeruhi akamatwa

TAKUKURU, Manispaa Ubungo Yawafikia Waendesha Bajaji, Bodaboda

Polisi Yatoa Onyo Kali Kwa Waganga wa Tiba Mbadala

TEA Kukarabati Jengo La Bodi Ya Maktaba Kwa Milioni 300

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Dirisha  La Udahili Awamu Ya Pili Lafunguliwa-TCU
Next Article Biashara Kati Ya Tanzania Na Uturuki Yapanuka Kwa Kiasi  Kikubwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Twendeni Tukapige Kura Ya Ukombozi, CHAUMMA Yahitimisha Kampeni
Habari October 28, 2025
Elimu Ya Nishati Safi Ya Kupikia Yawafikia Maofisa Dawati Ngazi Ya Mikoa Na Halmashauri
Habari October 27, 2025
Wananchi wahamasishwa kuandika historia mpya kupitia kura
Habari October 25, 2025
Shibuda: WanaMaswa jitokezeni kupiga kura bila woga
Habari October 25, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?