MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania Yapiga Hatua Kwenye Elimu ya Kidijitali Kupitia Ushirikiano na China
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania Yapiga Hatua Kwenye Elimu ya Kidijitali Kupitia Ushirikiano na China
Habari

Tanzania Yapiga Hatua Kwenye Elimu ya Kidijitali Kupitia Ushirikiano na China

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimezindua rasmi Kituo cha Ushirikiano wa Elimu ya Kidijitali kati ya China na Afrika ikiwa ni hatua kubwa ya kuimarisha elimu ya kisasa kwa kutumia teknolojia bunifu.
Habari Picha 9234
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma na Utafiti, Profesa Nelson Boniface, amesema kuanzishwa kwa kituo hicho ni mafanikio makubwa katika safari ya mageuzi ya elimu barani Afrika.
“Ni heshima kubwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa mwenyeji wa kituo hiki muhimu. Tunapitia zama za mabadiliko makubwa ya kiteknolojia, na ni wajibu wetu kuhakikisha walimu wetu wana ujuzi na uwezo wa kutumia zana za kisasa za kidijitali katika ufundishaji, hasa katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM),” amesema Profesa Boniface.
Amesema Kituo hicho kimeanzishwa kwa ushirikiano kati ya UDSM na Zhejiang Normal University ya China, kikilenga kukuza uwezo wa walimu na wakufunzi katika kutumia teknolojia ya kidijitali katika kufundisha na kujifunza.
Habari Picha 9225
Pia amesema mafunzo ya wiki moja yameandaliwa kwa walimu wa shule za msingi, sekondari, na wakufunzi wa vyuo, yakiwa na lengo la kuwawezesha kufundisha kwa mbinu bunifu na zinazokidhi mahitaji ya karne ya 21.
Habari Picha 9235
Profesa Boniface amekishukuru Chuo Kikuu cha  Zhejiang Normal kilichopo nchini China kwa ushirikiano thabiti, pamoja na Shule ya Elimu ya UDSM na Taasisi ya Confucius kwa maandalizi ya tukio hilo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Elimu ya UDSM, Dkt. Nkanileka Mgonda, amesema uzinduzi wa kituo hicho ni ushahidi wa dhamira ya pamoja ya kuleta mapinduzi chanya katika sekta ya elimu kupitia teknolojia.
Habari Picha 9226
“Kituo hiki kitakuwa kitovu cha ubunifu, mafunzo na majadiliano ya kitaaluma kati ya walimu wa Tanzania na wataalam kutoka China. Ushirikiano huu ni fursa ya kipekee kwa walimu wetu kupata ujuzi wa kisasa unaowandaa wanafunzi kwa dunia ya sasa na ya baadaye,” amesema Dkt. Mgonda.
Akizungumza kwa niaba ya Zhejiang Normal University, Huang Xiao ameeleza kuwa kituo hicho kinawakilisha mwanzo wa ushirikiano wa muda mrefu kati ya taasisi za elimu za China na Afrika.
Habari Picha 9227
“Walimu ndio msingi wa maendeleo ya jamii yoyote. Katika dunia ya sasa, ujuzi wa kidijitali si hiari tena bali ni hitaji. Kupitia mafunzo haya, tutashirikiana na walimu wa Tanzania si tu kwa maarifa, bali kwa kujenga uwezo endelevu wa kujifunza na kufundisha,” amesema Huang Xiao.
Ameongeza kuwa programu ya mafunzo itahusisha wataalam kutoka China katika nyanja za akili bandia, mbinu za kisasa za ufundishaji na elimu ya sayansi, huku akisisitiza kuwa ushirikiano huu unajenga daraja jipya la maendeleo ya elimu ya kidijitali kati ya China na Tanzania.
Uzinduzi wa Kituo cha Ushirikiano wa Elimu ya Kidijitali kati ya China na Afrika ni hatua muhimu katika kuleta mageuzi ya elimu nchini Tanzania. Kupitia ushirikiano huu, walimu wanapata fursa ya kujiimarisha kitaaluma, huku mfumo mzima wa elimu ukielekezwa kwenye matumizi ya teknolojia, ubunifu na ushirikiano wa kimataifa.

You Might Also Like

Trilioni 11.5 Zimetumika Miradi Ya Maendeleo Kigoma

Waziri Ridhiwani Awataka Wafanyakazi Kuongeza Bidii Katika Kazi

Wakumbushwa Kufuata Utaratibu Wa Kuboresha, kurekebisha sheria 

Tanzania Mwenyeji Mkutano wa Mafuta na Gesi, 2025

Japan Yatoa Bilioni 27 Kuboresha Sekta Ya Afya

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Roman Glorig Ahuisha Mkataba wa Uwakilishi wa Heshima wa Tanzania Nchini Czech
Next Article Dirisha  La Udahili Awamu Ya Pili Lafunguliwa-TCU
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CHAUMMA Kuunda Mamlaka ya Mazao ya Kimkakati – Salum Mwalim
Habari September 14, 2025
Heshima ya Udaktari Ni Mwito wa Kulitumikia Taifa: Dkt Ikomba
Habari September 14, 2025
Rais Wa CWT Suleiman Ikomba Sasa Ni Daktari
Habari September 13, 2025
Salum Mwalim: Nitarejesha Hadhi ya Kanda ya Ziwa na Kuinua Zao la Pamba
Habari September 12, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?