MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TARURA Yatoa Elimu Nane Nane
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TARURA Yatoa Elimu Nane Nane
Habari

TARURA Yatoa Elimu Nane Nane

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
DODOMA: WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeungana na taasisi nyingine za Serikali kushiriki Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuwafikia wananchi na wadau mbalimbali kwa kutoa elimu na kupokea maoni.
Akizungumza wakati wa maonesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa TARURA, Catherine Sungura amesema lengo kuu la ushiriki wa TARURA katika maonesho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu ya wakala huo, hasa katika usimamizi wa ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara mijini na vijijini.
“Tumejipanga kutoa elimu kwa wananchi juu ya maeneo mbalimbali tunayoyasimamia ikiwemo matengenezo ya kawaida ya barabara, uboreshaji wa maeneo korofi, shughuli za maabara, masuala ya mazingira na ushirikishwaji wa jamii,” amesena.
Amebainisha kuwa kupitia wataalamu waliopo kwenye banda la TARURA, wananchi wataelimishwa namna wanavyoweza kushiriki moja kwa moja katika shughuli za matengenezo ya barabara kupitia vikundi vya kijamii, hatua inayolenga kuongeza ushirikiano baina ya Serikali na wananchi katika kuboresha huduma za miundombinu.
“Tunawahamasisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea banda letu ili kupata elimu ya moja kwa moja kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana TARURA, hasa zile zinazolenga kuinua ushiriki wa jamii katika miradi ya barabara,” amesema.
Pia amewahimiza wananchi kutembelea banda la TARURA pamoja na mabanda mengine ya taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI, yaliyo katika hema maalum la “Government Zone Pavilion 2”, ambapo elimu zaidi kuhusu taasisi hizo inatolewa.

You Might Also Like

Umka yawashauri wakulima kutumia mbolea yake

Dkt Natu Mwamba Ashuhudia Utiaji Saini CRDB Na Taasisi Tatu Za Fedha Kimataifa

Mafua, Kifua Yadaiwa Kusababisha Kifo cha Job Ndugai

Masauni: Mapendekezo Ya Kulifanya NEMC Kuwa Mamlaka Yamepokelewa

Biteko Aiwakilisha Tanzania, Uapisho Wa Rais Boko, Botswana

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wakazi Wa Ntyuka Wataka Kiongozi Mchapakazi
Next Article Jaji Mwambegele: Habari Sahihi ni Msingi wa Ushiriki Mpana wa Wananchi Kura 2025
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?