MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yatumia Zaidi Ya Bilioni 100 Kupeleka Umeme Simiyu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yatumia Zaidi Ya Bilioni 100 Kupeleka Umeme Simiyu
Habari

Serikali Yatumia Zaidi Ya Bilioni 100 Kupeleka Umeme Simiyu

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage.
WAZIRI wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali kupitia wizara hiyo imetumia Sh. Bilioni 107.36 kupeleka umeme kwenye Vijiji vyote  474 vya Mkoa wa Simiyu.
Kapinga ameyasema hayo  wakati akitoa tathmini ya hali ya upatikanaji wa umeme Mkoa wa Simiyu na maendeleo ya usambazaji wa nishati safi ya kupikia wakati wa kuhitimisha ziara  ya kikazi ya Rais, Samia Suluhu Hassan Mkoani humo.
“Mheshimiwa Rais baada ya kumaliza upelekaji wa umeme kwenye Vijiji, hivi sasa tunapeleka umeme kwenye Vitongoji na hivi sasa tunatekeleza miradi ya umeme kwenye Vitongoji 638 kati ya Vitongoji 1,408 vya Mkoa wa Simiyu”, amesema.
Amesema Serikali itajenga kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Simiyu kupitia mradi wa gridi imara, pia hivi sasa Mkoa huo unapata huduma ya umeme kutoka Mikoa mitatu ya Shinyanga, Mwanza na Mara.
Amesema kituo hicho kitazidi kuimarisha hali ya umeme Simiyu na hivyo kuwa muhimu kwa maendeleo ya watu wa Simiyu.
Amesema mradi wa gridi imara  mkoani Simiyu una sehemu mbili ambazo ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Ibadakuli Shinyanga hadi Bariadi utakaojengwa kwa takribani Sh. Bilioni 48 na ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Bariadi kitakachojengwa kwa gharama ya Sh. Bilioni 49.
Amesema kukamilika kwa mradi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme Mkoa wa Simiyu utawezesha Mkoa kuwa na  uwezo wa megawati 150.
Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, Kapinga amesema Mkoa wa Simiyu umepata mitungi ya gesi ya  ruzuku takribani 16,275 ambayo yote tayari imeshachukuliwa na wananchi kwa bei ya ruzuku.

You Might Also Like

AUWSA Kutibu Maji Taka Yatumike Kwenye Kilimo

Matumizi Holela Ya Vilevi Hatari Kwa Watumiaji

Tume Ya Kurekebisha Sheria Tanzania Kuipitia Sheria Ya Takwimu

TUCTA Yakutana Na Mkuu Wa Mkoa Mbeya, Maandalizi Mei Mosi kitaifa 2025.

Wananchi Wachukue Hatua Iwapo Hawajaridhika Na Huduma-TCF

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article FAJ Yataka Wahamiaji Wa Kazi Wa Afrka, Wanaokwenda Maeneo Mengine Walindwe
Next Article PURA Yajipanga Gesi Asilia Itumike Kwenye Magari
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?