MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: UDSM Yatumia Teknolojia Ya Kidijitali Kukabili Sumukuvu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > UDSM Yatumia Teknolojia Ya Kidijitali Kukabili Sumukuvu
Habari

UDSM Yatumia Teknolojia Ya Kidijitali Kukabili Sumukuvu

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimetumia teknolojia ya kidijitali katika kukabiliana na tatizo la sumu kuvu.

Profesa kutoka Idara ya Sayansi na Teknolojia za Chakula, chuoni hapo, Lilian Kaale amesema hayo alipozungumza na Mfanyakazi Tanzania.

Amesema kwa kutumia teknolojia hiyo wameangalia zile hali zinazomfanya huyo mdudu ambaye anatoa sumu ambayo ndio sumukuvu na kuidhibiti.

“Teknolojia hii imewekwa sensa ambayo ina sensi joto, mvuke pamoja na unyevunyevu, hizi ni hali tatu kubwa kama hazijafikia kile kiwango cha wadudu kutoa sumu, hawatoi sumu. Kwa hiyo teknolojia ikianza kufikia kile kiwango kwa ajili ya kutoa sumu inakupa taarifa, pia inarudisha zile hali kuzuia wadudu wasizalishe sumu.

“Kwa hiyo ni teknolojia nzuri. tumeshaiweka kwenye ghala mojawapo la kuhifadhia lililopo eneo la Chemba Dodoma na sasa inafanya kazi,” amesema.

Amesema kwa hatua hiyo, wanaangalia ni jinsi gani wanaweza kuishauri serikali na kuandika sera kwa ufupi, kuona jinsi gani ya kuendeleza teknolojia iende kwenye maghala ya kuhifadhi chakula ambayo yako Tanzania.

Amesema tatizo hilo la sumukuvu linashambulia zaidi mahindi na karanga.

“Ukiangalia mahindi kila mtanzania anakula mahindi kwa maana nyingine ni kwamba tukiathirika kwenye mahindi tutapoteza nguvu kazi kubwa ya watanzania maana yake watakufa.

“Watakufa kwa kuwa sumu kuvu inaua inasababisha kansa ya ini na ukiangalia utafiti uliofanyika 2018 unaonyesha asilimia 8.2 ya vifo vinavyopatikana duniani vinatokana na kansa ya ini. Na sumu kuvu inachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha kansa ya ini,” amesema.

Profesa huyo amesema tatizo lililojitokeza Chemba mwaka 2015 na kuua baadhi ya watu ndilo lililomvutia kufanya utafiti huo.

Kwamba baada ya vile vifo vilivyotokea Chemba, serikali ilipeleka sampo Marekani pamoja na Belgium kupima kuona tatizo lilikuwa ni nini ikagundulika kuwa ni sumu kuvu hapo utafiti ukaanza kwa kasi nchini Tanzania.

Amesema hivyo nao chuo kikuu hicho wakaona wafanye utafiti huo kwa kutumia teknolojia hiyo ya kidijitali.

You Might Also Like

JAB Yatoa Mwezi Moja Kuthibitishwa, kupewa vitabulisho

Mfumo Uendeshaji Mashauri Kidigitali Kwa Watumishi wa Umma Uharakishwe

Dkt  Biteko ashiriki  Kikao Cha Mawaziri  wa Nishati  Uganda

Waziri Mkuu Majaliwa ndani ya SGR

Matukio Mbalimbali Katika Picha Baada Ya Waziri Mkuu Kuwasilisha Makadirio Ya Mapato Ya Bajeti

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Senene Waongezewa Thamani UDSM
Next Article Wanafunzi Kutoka Veta Kushiriki Mafunzo Japan
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?