MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Senene Waongezewa Thamani UDSM
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Senene Waongezewa Thamani UDSM
Habari

Senene Waongezewa Thamani UDSM

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: WADUDU aina ya senene wameongezewa thamani kwa kufanyiwa utafiti wa kutolewa mafuta ambayo hutumika kama dawa, kisha mabaki yake husagwa kwa ajili ya kupikia vyakula mbalimbali vya kuokWa ikiwepo keki.

Profesa Kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Idara ya Sayansi na Teknolojia za Chakula, Lilian Kaale amesema hayo katika Maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu inayohitimishwa leo Juni 11, 2025 chuoni hapo alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa Mfanyakazi Tanzania.

Amesema, “Sasa hivi ukila senene wakiwa bado hawajaongezewa thamani unakuta wana mafuta mengi sana na tukaona kwa nini tusitoe kwanza yale mafuta,

“Na tulichofanya hapa tumetoa mafuta, na hayo mafuta tumeyafanyia utafiti tukaona yana virutubisho vizuri sana kwa kifupi mafuta hayo yanatumika kama dawa sio mafuta ya kawaida,”.

Amesema mafuta hayo yana virutubisho vikubwa vitatu ambavyo ni Omega 3, Omega 6 na Omega 9, hivyo mtumiaji wa mafuta hayo hutumia kama dawa kwa kuchanganya kiasi kidogo na chakula kinapokuwa kimeiva tayari.

Virutubisho hivyo vinajenga mwili na vinaweka chembe chembe za mwili kuwa imara.

“Baada ya kutoa hayo mafuta yale mabaki ya senene yaliyobakia yakatengenezwa unga, huo unga mtu akitaka kutumia anaweza kuchanganya na unga wa mahindi akatengeneza uji au unachukua, unachanganya na unga wa ngano unatengeneza mikate, biskuti, na bidhaa nyingine. Kwa hiyo mtu akila anakula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha.

“Kwa hiyo kwa haraka utaona kilo moja ya senene inaweza ikanufaisha mkulima, jamii au mtu mmoja mmoja kwa kiasi kikubwa kwa kuwa chupa ndogo ya ujazo 200 mafuta yake ni sh 20,000 kwa sababu ya hivyo virutubisho vilivyopo,” amesema.

Amesema wamebuni mradi huo wa wadudu hao wanaopatikana mkoani Kagera kwa kuwa hakuna mtu aliyeongeza thamani kwenye hao senene.

Amesema kama watafiti na wabunifu lengo lao ni kutafuta majawabu ya matatizo katika jamii, na wanavyotafuta matatizo hayo na kuyathibitisha kinachofuata ni kutafuta wawekezaji wanaoweza kuichukua hiyo teknolojia ili wazalishe kwa wingi na kuuza kwenye jamii.

You Might Also Like

Tari Ilonga yaboresha mbegu, mavuno yapanda hadi tani 3.8 kwa hekta

LHRC Kushirikiana  Na JOWUTA Kuwajengea Uwezo Wanahabari Katika Masuala Ya Haki Zao Na Sheria Za Kazi

Rais Samia Afungua Barabara Ya Mbinga-Mbamba Bay Yenye Km 66-Ruvuma

GIZ, IUCEA waratibu uchambuzi wa data kidijitali kwa wahitimu

Wananchi Wachukue Hatua Iwapo Hawajaridhika Na Huduma-TCF

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article OSHA Yatoa Gawio Kwa Serikali Zaidi  Ya Bilioni 10
Next Article UDSM Yatumia Teknolojia Ya Kidijitali Kukabili Sumukuvu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Fema Mining & Drilling Mfano wa Kuigwa – Musukuma
Habari September 23, 2025
Mgodi Wa Dhahabu Wa Nyanzaga Kunufaisha Wananchi, Ujenzi Wazidi Kupaa
Habari September 23, 2025
Sekta Ya Madini Yazidi Kuchangia Ukuaji Wa Uchumi – Majaliwa
Habari September 23, 2025
Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?